SUA KUANZISHA MASHINDANO YA BUNIFU KWA WANAFUNZI KUBORESHA KILIMO NCHINI


Na Christina Cosmas, Morogoro

CHUO kikuu cha sokoine cha kilimo (SUA) kwa ushirikiana mashirika ya maendeleo ya kilimo kutoka nchi mbalimbali ikiwemo USAID, TAOTIC pamoja USDA wameanzisha mashindano ya kusaka ubunifu kwa vijana katika kusaidia wakulima kuboresha kilimo hapa nchini.

Mkurugenzi msaidizi wa sayansi na teknolojia kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia Alexander Mtawa amesema mashindano hayo yanayoendeshwa kupitia mradi wa YEESI LAB yanayohusisha vijana wabunifu kwenye masuala ya kilimo yamelenga kuwapa utayari vijana kubuni teknolojia rahisi itakayowasaidia pia wakulima wadogo hususani walioko vijijini.

Akizungumza kwenye mashindano hayo, mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima amewataka vijana wanaoshiriki shindano hilo kuwa na ushirikiano na ubunifu katika kuhakikisha kazi zao zinakubalika katika jamii ili kuleta tija inayokusudiwa ikiwemo kufungua viwanda na kuongeza ajira kwa vijana huku wakongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo.


Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vijana hao ambao watakuwa ni muhimili mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao na kuboresha suala la kilimo ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.

Akizungumzia mradi huyo mkuu wa mradi huo Dk. Kadeghe Fue kutoka SUA alisema kuwa vijana wote watakaoshiriki shindano hilo na kufanikiwa watanufaika zaidi na masuala ya teknolojia na ubunifu katika kilimo ikiwa ni pamoja na kujipatia kipato chenye tija kwao na familia zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post