Tazama Picha : KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA MKOA WA SHINYANGA... JAJI MAHIMBALI ATAKA SHERIA ITUMIKE KUPATA HAKI


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria. Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga kimefanyika leo Alhamisi Februari 1,2024 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali na Mgeni wa Heshima akiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme - Picha na Kadama Malunde & Marco Maduhu

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali, amewataka wananchi katika Mkoa wa Shinyanga na Simiyu, kuitumia vyema elimu ambayo wameipata kwenye Maadhimisho ya wiki ya sheria, kwamba iwe chachu ya maboresho ya mtindo wa maisha yao kisheria na kijamii, na kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Amebainisha hayo leo Februari 1,2024 kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya sheria nchini, ambayo yalianza kutolewa Januari 24 hadi 30 mwaka huu, Maadhimisho ambayo mkoani Shinyanga yamefanyika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.


Amesema katika Maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria nchini, wananchi wamepewa elimu mbalimbali za kisheria na kujengewa uelewa wa kutosha, hivyo imani yao kama Mahakama ni kuona wananchi wanabadilika katika mtindo wao wa maisha na kutafuta haki kwa mujibu wa sheria na siyo kujichukulia sheria mkononi.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali.

“Elimu ambayo wananchi mmeipata katika Maadhimisho ya wiki ya Sheria isiishie kwenye Mabanda ya Maonyesha, bali iwechachu ya Maboresho ya Mtindo wa Maisha yenu Kisheria na Kijamii, na siyo kujichukulia sheria mkononi vitumieni vyombo vya utoaji haki kupata haki zenu,”amesema Jaji Mahimbali.


“Mfumo wa Sheria na uwepo wa Mahakama umechangia kwa kiasi kikubwa sisi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla kuendelea kuwepo na umoja, hebu fikiria maisha haya kusingekuwepo na Sheria ingekuwaje,… si amani isingekuwepo kungekuwa na vurugu tu, tutumieni sheria kupata haki,”ameongeza.

Aidha, amesema Mahakama zote mkoani humo pamoja na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, wamejipanga vyema kufanya kazi kwa spidi ya usikilizaji wa mashauri, na kwamba hadi kufikia june mwaka huu Mashauri yote ya nyuma 275 yatakuwa yamekwisha sikilizwa, ili waanze kusikiliza mashauri ya mwaka huu 2024.
Katika hatua nyingine, amewataka Mahakimu kuzingatia viapo vyao, Miiko na Madili ya Taaluma yao katika utendaji kazi, na kwamba Mahakama haitakuwa na huruma kwa Hakimu ambaye anatakwenda kinyume na maadili ya kazi au kuzembea kazini, bali wafike Ofisini kwa wakati na kuwahudumia wananchi na kutenda haki.

Naye Wakili wa Serikali Solomoni Rwenge akisoma Risala kwenye kilele cha Maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria, amesema utoaji haki ni nguzo Muhimu kwa Taifa, huku akiwataka wadau wote wa utoaji haki wajitathimini juu ya utoaji haki kwa wananchi na kwa njia ya ukweli.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) mkoani Shinyanga Shabani Mvungi, akisoma Risala ya Mawakili wa kujitegemea, pamoja na mambo mengine kwamba wataendelea kuboresha Mahusiano Mazuri na wadau wa haki jinai, pamoja na kuendelea kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi, pamoja na kuwapatia elimu ya sheria na masuala ya haki jinai.

Ametoa pia pongezi kwa Mahakama kwa kupiga hatua kubwa katika Matumizi ya Teknolojia na kuimarisha upatikanaji wa haki.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, akitoa salamu za Serikali, amesema wataendelea kuboresha mazingira mazuri kwa vyombo vya utoaji haki ikiwamo ujenzi wa majengo mazuri, na kwamba kwa sasa wameshajenga Jengo la ghorofa la Ofisi ya Taifa ya Mashitaka.

Aidha, ameitaka Mifumo Jumuishi iendelee kusomana ili haki ipatikane kwa haraka, na kwamba utoaji haki kwa haraka utaondoa Malalamiko kwa wananchi.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini mwaka huu 2024 inasema "Umuhimu wa dhana ya haki kwa Ustawi wa Taifa, nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo wa haki jinai"
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa salama za Serikali kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.
Meza kuu wakifuatilia matukio

Wakili wa Serikali Solomoni Rwenge akisoma Risala kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria.
Mwenyekiti wa TLS Shinyanga Shabani Mvungi akisoma Risala kwenye Maadhimisho ya wiki ya Sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi cha Katibu Tawala wa Mkoa huo kutokana na kuonyesha mchango wake wa Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kwa mchango wake wa Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Shinyanga kama mdau wa Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga kwa mchango wake wa Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa mchango wake wa Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Benki ya CRDB kwa mchango wake wa Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Jambo FM kwa mchango wake wa kuandika habari za Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Malunde 1 Blog kwa mchango wake wa kuandika habari za Mahakama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa AZAM kwa mchango wake wa kuandika habari za Mahakamani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa cheti cha pongezi kwa Gazeti la NIPASHE na Shinyanga PRESS CLUB BLOG kwa mchango wake wa kuandika habari za Mahakamani.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali awali akikagua Gwaride katika maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria.
Askari Polisi wakiwa katika Gwaride.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali awali akikagua Gwaride katika maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria.




Tazama Picha zaidi Matukio yaliyojiri wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga




Picha za kumbukumbu

Picha zote na Marco Maduhu na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post