WANANCHI JITOKEZE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA-MBUNGE CHEREHANI





Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga Emmanuel Cherehani akizungumza jambo na mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mbika Kata ya Ushetu .



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Wazohuru Mathias Canal akizungumza na wananchi wa kata ya Ulowa Shinyanga ikiwa ni ziara ya kikazi ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga Emmanuel Cherehani








Na Mathias Canal, Ushetu-Kahama


Wananchi wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2024.


Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga Mhe Emmanuel Cherehani ameyasema hayo tarehe jana wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mbika Kata ya Ushetu na Kijiji cha Ilomelo kata ya Ulowa.


Mbunge Cherehani pia amewahamasisha vijana na akina mama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo ili kuleta mabadiliko katika jamii.



"Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan toka ameingia madarakani tumeona mambo makubwa ya kimaendeleo aliyoyafanya. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani akina mama walivyo na uwezo mkubwa katika uongozi. Nichukue nafasi hii kuwahamasisha mama zangu, dada zangu pamoja na vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa pindi mchakato utakapotangazwa rasmi," amesema Mbunge Cherehani.



Cherehani pia amewataka wananchi kuchagua viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaotaka kuwatumikia kweli kwa kuwaletea maendeleo huku akiahidi kuendelea kushirikiana na viongozi waliopo kuhakikisha wanaendelea kuboresha maisha ya wananchi katika Jimbo hilo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post