TBS YAKUTANA NA WADAU WA MABATI NA MALIGHAFI KANDA YA MASHARIKI

Mkurugenzi wa Uaandaji wa Viwango Bw. David Ndibalema ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TBS, akifungua kikao cha Wadau wa bidhaa za mabati nchini kilichofanyika leo Januari 17,2024 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

***************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limefanya kikao na wadau wa bidhaa za mabati nchini chenye lengo la kujenga uelewa ili kuweka mikakati mahususi kwa bidhaa za mabati zinazozalishwa na kuingizwa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 17,2024 katika ukumbi wa TBS Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uaandaji wa Viwango Bw. David Ndibalema ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TBS, amesema kuwa katika kuunga juhudi za serikali TBS inaendelea kuwajibika ili kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinazotoka nje ya nchi zinakidhi vigezo vya ubora.

Aidha Bw. Ndibalema ametoa wito kwa wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nje ya nchi kuhakikisha bidhaa hizo zinakidhi Viwango vya ubora ili kuondokana na malalamiko na kulinda thamani ya fedha kwa wateja.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Sheria, Ukaguzi na Ufuatiliaji Dkt,Candida Shirima amesema kuwa TBS inapokuwa ikitekeleza majukumu yake kisheria inautaratibu wa kukutana na wadau wake  ili kukumbushana matakwa ya kisheria katika masuala mbalimbali likiwemo la viwango vya ubora.

Mkutano huo umelenga kugusia masuala mbalimbali kuhusiana na uagizaji wa bidhaa za mabati nchini pamoja usambazaji wa bidhaa hizo ili kuhakikisha bidhaa hizo zinakidhi matakwa ya ubora.
Mkurugenzi wa Uaandaji wa Viwango Bw. David Ndibalema akizungumza katika kikao cha wadau wa bidhaa za mabati nchini kilichofanyika leo Januari 17,2024 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Sheria, Ukaguzi na Ufuatiliaji Dkt,Candida Shirima akizungumza katika kikao cha wadau wa bidhaa za mabati nchini kilichofanyika leo Januari 17,2024 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Bw.Francis Mapunda akizungumza katika kikao cha wadau wa bidhaa za mabati nchini kilichofanyika leo Januari 17,2024 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wadau wa bidhaa za mabati nchini wakiwa kwenye kikao na TBS kilichofanyika leo Januari 17,2024 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post