TANI LAKI 1.5 ZA KOROSHO ZASAFIRISHWA KUPITIA BANDARI YA MTWARA


Tani 150,000 za Korosho ghafi zimesafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutumika kikamilifu kwa Bandari hiyo kusafirisha korosho zote ghafi zinazolimwa Katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania( TPA) Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi amesema tangu kuanza kwa msimu wa korosho Bandari hiyo imehudumia Meli zaidi ya 18 za makasha, Meli tatu zikiwa zimeleta makasha matupu na Meli 15 zimesafirisha Korosho ghafi.

“ Mpaka sasa tumeshasafirisha tani laki moja na nusu na mpaka mwishoni mwa Januari tutakuwa tumeshasafirisha tani laki mbili. Tunakushukuru sana Serikali kwa maelekezo yake ambayo yameongeza ufanisi wa Bandari.” Amesema Nyathi.

Aisha amewashukuru Wadau wa Bandari na kampuni ambazo ziliamua kuwekeza katika Bandari hiyo ikiwamo Kampuni ya kuhudumia Makasha ya CMA na kampuni ya Meli ya Mediteranian Shipping kwa kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha usafirishaji wa korosho ghafi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post