TANESCO YASHIRIKI MAONESHO YA 10 YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZANZIBAR


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeshiriki kwenye maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar.

Maonesho hayo yamezinduliwa Januari 10, 2024 na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi, ambapo alizipongeza Taasisi zote ziizoshiriki katika maonesho hayo.

Ushiriki wa Tanesco katika maonesho hayo ni kupata nafasi ya kukutana na wadau , ikiwemo wawekezaji pamoja na fursa za kibiashara ambapo sambamba na kutoa huduma bora za Umeme , Tanesco pia imejipanga kujiendesha kibiashara.

Maonesho hayo yana washiriki zaidi ya 500 na yamebeba kauli mbiu isemayo "Biashara mtandao kwa maendeleo ya Biashara na Uwekezaji"

TANESCO inawakaribisha wakazi wote wa Zanzibar, Pemba na maeneo jirani katika banda lao la maonesho lililopo katika viwanja vya Fumba, Zanzibar kuanzia tarehe 7-19, Januari 2024 ili kujifunza miradi ya kimkakati inayoendelea, fursa za uwekezaji kwenye miradi ya umeme na huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post