KADA WA CHADEMA AJIUNGA CCM, AELEZA ALIYOYAISHI CHADEMA

Na Dotto Kwilasa,DODOMA.


KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt,Emanuel Nchimbi amepokelewa jana
katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM akiwa na zawadi maalumu kwa wana CCM.


Akizingumza kwenye mapokezi hayo, Nchimbi aliwaambia umati wa wana CCM kuwa amewaletea zawadi ambayo ni wanachama wapya watatu wa CHADEMA akiwemo kada maarufu Upendo Peneza.


Amesema kama Chama watakuwa mstari wa mbele kutaka maridhiano na Vyama pinzani huku akiwataka wanaCCM kubishana na Vyama vya upinzani kwa hoja ili kujitofautisha kutokana na ukongwe Wake.


Dkt, Nchimbi amesema kila mwana chama anatakiwa kujua umuhimu wake ndani ya chama kuanzia ngazi za mashina hadi taifa.


" Tukumbuke kuwa chama ni wana chama na ndio maana kazi ya kukitangaza ni ya wanachama wenyewe, "Alisema Dkt Nchimbi


" Niwaombe Sana waana CCM kakitangazeni chama kwa ni hakuna mwenye uchungu na chama chake kama mwanachama mwenyewe chukueni dhima hiyo Kutakana kukitangazani chama kwa hoja nasio kwa ushabiki kitofautisheni chama kikongwe hivi vyama vinavyochipukia, "amesisitiza


Aidha amewataka wanachama wote kuanzia ngazi ya Shina kuhakikisha wanakitetea na kukisemea Chama vizuri kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na chama hicho.


Kwa upande wake Kada wa CHADEMA Upendo Peneza amesema ameamua kuhamia CCM, kutokana na Rais Samia kuweka mazingira Mazuri kwa vyama vya Siasa, wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu kuweka mazingira ya Umoja wa kitaifa kwa kukubali kukaaa pamoja kwa ajili ya Maridhiano.


Kada huyo Mpya wa CCM, aliyehama Chadema aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum na mwenzake aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Manyara, Benson Andrew pamoja na Onesmo Mbuya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wilayani Morogoro.


Akizungumzia Chama chake cha awali Peneza amesema,"Nilijiunga na chadema kwa sababu nilikuwa na kiu ya mabadiliko ya nchi yetu kwa miaka 15,kwa miaka 15 nilitamani mabadiliko lakini kiu yangu haikutekelezwa, "amesema na kuongeza,;


Kile sio chama cha kutafuta mabadiliko ya watanzania,hebu tuambizane hapa tu ukweli hivi kweli huwa mnatuelewa? Alihoji


Rais alitamka kuwaunganisha watanzania na kuleta mageuzi na ndicho alichokifanya
kwa kuanzisha safari ya maridhiano ambayo ilikufa ikaanza upya lakini CHADEMA walikataa kuingia kwenye mazungumzo ndipo Rais akaanzisha vikao na viongozi wetu na wengi walio kuwa kizuizini waliachiwa na tulikuwa tumesusia ruzuku lakini rais alitupa , "ameeleza


Anafafanua kuwa pamoja na chama chake kupewa pesa nyingi za ruzuku lakini bado hakikuweza kumiliki ofisi za chama na kwamba zilizopo sasa zimetokana na ruzuku ambayo imetolewa na serikali.


"Tulikuwa hatuna Uhuru wa kufanya mikutano lakini sasa ameirudisha jambo moja na kubwa la kujifunza kwake kama mengine yakitushinda ni kuwa mvumilivu na mstahimilivu, " Amesema


Licha ya hayo ameeleza utovu wa nidhamu miongoni mwa wana CHADEMA kuwa hata Rais Samia alipokubali kuingia nao kwenye maridhiano , ndani ya mikutano walitumia kumsema na kumdhihaki kwa lugha zote za kihuni lakini jambo ambalo Mama Samia hakulibeba na badala yake aliendelea kuwasikiliza.


"Kama kuna kiongozi basi Rais Samia ni msikivu, amekuwa chachu ya mabadiliko ya kweli kupitia kumchagua katibu Mkuu anayeendana na demokrasia na kuheshimu haki za wananchi,kwa ujumla alimchagua Katibu Mkuu mwenye viashiria vya demokrasia, " alisema


Akizingumzia maana na uhalisia wa Vyama vya upinzani amesema,"Vyama vya upinzani kwa asili ni watch dog ya demokrasia(wasimamizi) lakini leo inachukuliwa ni tofauti ,ukifuatilia kwa ndani unaumiza kichwa kwa sababu leo hii watch dog nae anahitaji watch dog, "alisisitiza


Ameongeza kuwa wapinzani wamekifanya chama kama sehemu ya kufanikishia biashara zao na kuwafanya wananchi kuwa bidhaa yao jambo ambalo kwa sasa haliwezi tena kuendelea kwa sababu Wananchi nao wamegundua sasa umuhimu wa umoja na wanaanza kurudi nyuma.


Kuhusu mwenendo wa maandamano Peneza amesema wananchi wanapaswa kujipambanua kwa kuwa wana siasa wanataka kuwatumia kama kipimo cha kujua biadhaa waliyobaki nayo(kama bado wanakubalika).


Amedai kuwa ili kuchochea maandamano hujikuta wanatumia hoja nzuri kama nyenzo kwao ili kuwaingiza watu barabarani kumbe lengo lao ni kutaka kujua wana watu wangapi na soko lao likoje kwenye jamii.


"Wanefanya ulaghai sasa wamenogewa, wameshtuka lakini wamechelewa,nasema haya maneno kwa sababu Lisu alitangaza maridhiano yamevunjika lakini viongozi wengine walimkana lakini juzi Mwenyekiti wa chama kasa hakuna maridhiano,ni mvurugano wa hali ya juu hakuna masikilizano, " Alisema na kuongeza;


Hivi karibuni Mbowe kwa mbwembwe alitangaza kuwa Rais alimpa milioni 150 kama mchango,kwa lugha nyingine niseme kwamba alikuwa na nafasi ya kuzungumza na Rais bila kuingia kwenyw maandamano,kitu ambacho naomba mkielewe ili mambo yaweze kutendeka inategeneana na kiongozi wa juu walivyo, "anasema


Amesema kuwa,"Haya maandamano yalibidi yaje baada ya bungee kumaliza kazi yao na sio kuwashinikiza watu kuandamana wakati hujajua bunge litaamua nini,ni kweli kuna ugumu wa maisha, vitu vimepanda bei lakini kuna mazungumzo kwa nini tusimpe mda wa majaribio, "alihoji kada huyo.


Kwa upande Wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uchapa kazi Wake huku akishukuru kwa miradi ya kimkakati inayotekekezwa Dodoma ikiwemo ujenzi wa Standard gauge.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments