AMUUNGUZA KWA MAFUTA YA MOTO JIRANI KISA KWANINI AMEIGA KUSUKA MTINDO WAKE WA NYWELE


Mkazi wa Nairobi, nchini Kenya amemmwagia mafuta ya kukaangia samaki jirani yake kwa madai ya kumuiga kusuka mtindo wa nywele.


Mkazi huyo aliyetambulika kwa jina la Catherine Wanjiru, amedaiwa kummwagia mafuta yaliyochemka, Sherry Nyanchomba, kisha kumtengua taya na kuvunja meno.Tukio hilo limetokea Januari 16, 2024 kwenye makazi yao huko Dandora, Nairobi, hii ni kwa mujibu wa Tovuti ya Citizen ya nchini humo.


Inaelezwa kwamba Nyanchomba alikuwa akirejea nyumbani usiku ndipo alipokutana na Wanjiru mlangoni ambapo alimshutumu kumuiga mtindo wake wa nywele.


Baada ya kumshutumu inaelezwa Wanjiru alikwenda kuchota mafuta ya moto yaliyokuwa karibu na kudaiwa kuyamimina usoni kwa Nyanchomba kabla ya kuanza kupigana.


Wanjiru alikamatwa na baada ya Polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo, alipandishwa kizimbani ambako alikana mashtaka, kisha kuachiwa kwa dhamana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments