MPC YALAANI KITENDO CHA WAANDISHI WA HABARI KUCHEKELEA KUPEWA NYAMA NA MBUNGE
TAARIFA KWA UMMA JUU YA UVUNJIFU WA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC), ni klabu iliyosajiliwa kwa sheria ya Society Act Mwaka 1994 na kupewa namba ya usajili ya SO 8262, ikiwa na dhima kuu ya kusimamia weledi wa uandishi wa habari ndani ya Mkoa wa Mwanza.

MPC imefuatilia kwa ukaribu kusambaa kwa kipande cha picha nyongefu kikionesha Mwandishi wa Habari Emmanuel Twimanye akimshukuru Hamisi Mwagao Tabasamu Mbunge wa Jimbo la Sengerema kwa kutoa mgao wa nyama ya Mbuzi na Kondoo kwa baadhi ya waandishi wa habari wa Wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, tukio lililotokea Januari 1, 2024.


MPC inalaani kitendo hicho kwa kuwa, kinakiuka misingi na maadili ya uandishi wa habari kwani Mwandishi wa Habari hatakiwi kupokea pesa, zawadi au bakishishi yoyote ile kutoka kwa Mwanasiasa, Afisa wa Serikali au Mfanyabiashara ili kuepuka mgongano wa kimaslahi kwenye utendaji kazi wake.


MPC inalaani kitendo hicho na imechukua hatua za kuwaonya waandishi wote waliohusika kwenye tukio hilo na kuwaelimisha athari za vitendo hivyo kwenye tasnia ya habari na mtazamo wa jamii na inawataka waandishi wote kuzingatia maadili ya uandishi wa habari kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Ahsanteni

Edwin C. Soko
Mwenyekiti, MPC
02.01.2024


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post