GOD FIRST DRIVING SCHOOL YATUMIA WIKI YA SHERIA KUTANGAZA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA, MIZIGO NA VIONGOZI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisoma kipeperushi chenye alama za usalama barabarani alipotembelea Banda la shule ya Udereva ya ‘God First Driving School’ ambacho ni Wakala wa Arusha Technical College wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga Jumamosi Januari 27,2024 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Anaripoti Kadama Malunde

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Mndeme amekipongeza chuo hicho kwa kutoa mafunzo ya udereva hali ambayo itasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Akizungumza wakati wa maonesho hayo, Meneja wa Masoko na Mahusiano wa God First Driving School, Masoud Mmanywa amewakaribisha wazazi, walezi na watu wote kujiunga na shule hiyo ya udereva ili wapate elimu bora ya usalama barabarani wakitumia kauli mbiu ya ‘Tanzania bila ajali inawezekana, timiza wajibu wako’.

Amesema Shule ya Udereva ya ‘God First Driving School’ inatoa mafunzo ya udereva wa magari ya abiria, mizigo na viongozi katika mkoa wa Shinyanga kinapatikana eneo la Butengwa, kata ya Ndembezi karibu na shule ya Sekondari KOM, barabara ya kuelekea Old Shinyanga.

Amezitaja kozi zinazofundishwa katika shule ya God First Driving School yenye namba za Usajili TRD/A.21/SHY/2020/028 ni pamoja na Kozi ya Udereva wa magari ya abiria (PSV daraja C, C1,C2 na C3) , Kozi ya Udereva wa magari ya mizigo (HGV daraja E) , Kozi ya udereva wa magari ya viongozi (V.I.P), Kozi ya udereva wa awali (Basic driving course daraja B na D) na Kozi ya udereva wa Bajaji na Pikipiki A na A2.

“Mafunzo yote yanafanyika chuo kila siku Jumtatu hadi Ijumaa kwa vitendo na siku ya Jumapili saa 9:00 alasiri darasani. Pia kwa wanafunzi waliopo vyuo mbalimbali hapa Shinyanga pamoja na waajiriwa watapatiwa mafunzo bila kuathiri ratiba zao ili waweze kujiongezea thamani katika soko la ajira”,amesema.

Wasiliana na God First Driving School iliyopo Butengwa Shinyanga Mjini kwa simu namba +255 625 966 084 au +255 757 437 829 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisoma kipeperushi chenye alama za usalama barabarani alipotembelea Banda la shule ya Udereva ya ‘God First Driving School’ ambacho ni Wakala wa Arusha Technical College wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga Jumamosi Januari 27,2024 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Meneja wa Masoko na Mahusiano wa God First Driving School, Masoud Mmanywa (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kuhusu mafunzo wanayotoa ya udereva wa magari ya abiria, mizigo na viongozi.
Meneja wa Masoko na Mahusiano wa God First Driving School, Masoud Mmanywa (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kuhusu mafunzo wanayotoa ya udereva wa magari ya abiria, mizigo na viongozi.
Meneja wa Masoko na Mahusiano wa God First Driving School, Masoud Mmanywa (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kuhusu mafunzo wanayotoa ya udereva wa magari ya abiria, mizigo na viongozi.
Wawakilishi wa shule na vyuo mbalimbali Mkoani Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu na meza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga Jumamosi Januari 27,2024 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post