ZIWA VICTORIA CHANZO CHA MAJI YA UHAKIKA KWA VIJIJINI 33 WILAYA YA BUNDA

Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa Ziwa Victoria linakwenda kuwa chanzo Cha maji kwa Vijiji 33 vya Wilaya ya Bunda na kufanya upatikanaji wa huduma ya Maji kuwa wa uhakika masaa 24 .


Mhandisi Mahundi amesema mtaalam Mshauri amekamilisha usanifu wake na pia serikali katika kuendelea kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji ina mpango wa kutoa maji kutoka Tanki la Maji Butiama lenye ukubwa wa lita milioni 2.5 katika Mradi wa Majisafi Mugango-Kiabakari kupeleka Nyamuswa kupitia Bisarye.

Mipango hiyo amebainisha akiwa katika Ziara Yake ya kikazi wilaya ya Bunda ya kutembelea mradi wa maji unaotekelezwa kwa kutumia chanzo Cha ziwa Victoria kwenye kijiji cha Tiring'ati.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini Mheshimiwa Boniface Getere ameishukru Serikali kwa uamuzi wa kutumia chanzo cha maji cha uhakika cha ziwa Victoria ili kuboresha huduma ya maji kwenye Wilaya ya Bunda.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post