WANAHARAKATI WA JINSIA WATAKIWA KUFANYA KWA VITENDO MAFUNZO WANAYOPEWA


MKURUGENZI Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi.Lilian Liundi amewataka wadau wanaohudhuria mafunzo ya semina za jinsia na maendeleo(GDSS) kuwa watetezi wa kwanza katika kupigania usawa Kijinsia na kukemea vitendo vya ukatili hadharani kutokana na yale wanayo jifunza.

Ameyasema hayo Desemab 15,2023 Mabibo-Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanaharakati wa Jinsia katika ofisi za mtandao wa Jinsia nchini amesema anatamani akiona mtu aliyealikwa na kuhudhuria semina hizo mara kwa mara akiwajibika kwa vitendo katika utetezi wa masuala yenye mlengo wa Kijinsia ili kuleta matokeo chanya ya semina hizo.

"Natamani kila anayekuja hapa atoe hesabu ya kile alichojifunza amefanyia nini amegusa maisha ya watu wangapi sio suala la kwenda Dar es saalam tusipoteze wakati huu kwani ni rasilimali za nchi na pesa zinazo tumika kufanya mikutano hii ni nguvu za walipa Kodi wa nchi flani na serikali yetu imeweka mkono wake wanatamani waone yale tulisema tutayafanya", amesema Liundi.
 
Aidha ameeleza kuwa wanapaswa kuleta mrejesho wa nini kimefanyika katika vipindi tofauti tofauti kwa wale watu ambao wana uhitaji wa taulo za kike mashuleni,wanao fanyiwa ukatili sehemu mbalimbali ambapo itaonesha kwa namna gani wametoa elimu.

Mwakilishi wa Idara ya uwezeshaji na Mafunzo,Bi Lina Sangai amesema kuwa wametoa mafunzo ambayo ni muendelezo wenye lengo la kutambua nini wamepata kujifunza wanapokua wakifundisha watu wengine na changamoto wanazo zipitia wakati wakitoa mafunzo ili kutatua changamoto zitakazo jitokeza

Naye Mwanaharakati wa jinsia kutoka mkoa wa Mara,wilaya ya Tarime Bi.Noela Joseph amesema kuwa ametumia muda wake kutoa elimu kwa jamii inayo mzunguka ili wanapojitambua na changamoto zitakapo jitokeza wapate sehemu ya kukimbilia.

"Kuna mtoto aliozwa akiwa na umri mdogo kwa maana alikua ni mwanafunzi wakataka kumkatiza ndoto zake baada ya matokeo kuwa yametoka amefaulu lakini wazazi walikua wameshapokea mahali lakini huyo mtoto tuliweza kupata taarifa na kumnusuru amerudi shule na mpaka sahivi anaendelea na shule" Bi. Noela amesema.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa yana kwenda kuwapatia wakufunzi uwezo ambao watakwenda kutoa mafunzo katika mikoa mikoa nane ya Tanzania kwa wanaharakati walio katika vituo vya taarifa na yanafanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Global affairs Canada.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post