ORYX YAUNGANA NA JAMII KUWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG

 


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole kwa wananchi wa Hanang waliofikwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha vifo na majeruhi huku ikitumia nafasi hiyo kukabidhi mitungi ya gesi 200 yenye ujazo wa kilo 15 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo kupata nishati safi ya kupikia.

Mitungi hiyo ya gesi na majiko yake ambayo imetolewa naql Oryx imekabidhiwa kwa Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga.

Akizungumza wakati wa kupokea mitungi hiyo Waziri Mhagama ameishukuru kampuni ya Oryx kwa mchango wake kwa wananchi wa Hanang kwani umekuja wakati muafaka kusaidia wananchi hao kwa kuwapatia nishati safi ya kupikia katika wakati huu mgumu.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mauzo Oryx Gas Shaban Fundi amesema kampuni hiyo imefika Hanang eneo la Katesh kuungana na kuwapa pole watanzania wenzao waliofikwa na janga la mafuriko na maporomoko. 

"Tunajua kwa hakika wenzetu wameathirika sana katika kipindi hiki ni gharama kubwa kupata vyanzo vya moto kupikia. Oryx Gas tumekuja kukabidhi majiko 200 na mitungi ya gas ujazo wa kilo 15 kwa waathirika wa tukio hili.

"Oryx Gas tunawaombea marehemu wapumzike kwa amani, zaidi tunawaombea majeruhi wote wapone haraka na werejee katika majukumu yao ya kila siku."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post