DCEA YATOA WASAIKOLOJIA SITA KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG


NA. MWANDISHI WETU

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) imetoa wataalam sita wa saikolojia na masuala ya ustawi wa jamii ambao wameungana na wataalamu wengine kutoa huduma katika kambi tatu za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe Hanang mkoani Manyara.

Akipokea wataalam hao, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi, amesema kutokana na maafa yaliyowapata waathirika hao ambao wamepoteza ndugu na mali zao na kupata msongo wa mawazo na hivyo wanahitaji kujengwa kisaikolojia kwa kuwapa matumani ili kuendelea kuishi na kurejea katika hali yao ya awali.

Pamoja na hilo Katibu Mkuu Yonaz amempongeza Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo kwa hatua hiyo kwa kusema timu ya DCEA itaungana na wataalam wengine waliopo kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia wananchi kwa kuwapa huduma ya unasihi (ushauri) pamoja na elimu ya kujikinga na magonjwa ya afya ya akili wanapoendelea kuhudumiwa na Serikali.

“DCEA imetoa Wasaikolojia hawa ambao watajikita kutoa elimu kwa waathirika wa maafa yaliyotokea, hii ni hatua nzuri kwa kuwafikia na kuwashauri pale inapobidi ili kusaidia kutopata msongo wa mawazo na kupambana na changamoto ya afya ya akili,” amesema Dkt. Yonazi

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka Bw. Daniel Kasokola, amesema Kamishna Jenerali wa Mamlaka amechukua hatua ya kutuma timu hiyo kama sehemu ya kutekeleza wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwataka watanzania wote kuungana kuwataidia wahanga hao na anaamini kuwa, timu hii kwa kushirikiana na wataalam nyingine itaaidia waathirika wa maafa hayo ili warejee katika hali zao za kawaida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post