BENKI YA CRDB YATANGAZA NEEMA KWA BODABODA, BAJAJIMKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa halfa ya kugawa zawadi ya Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi iliyokwenda sambamba na ugawaji wa Riflect kwa Waendesha Bodaboda iliyofanyika kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa halfa ya kugawa zawadi ya Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi iliyokwenda sambamba na ugawaji wa Riflect kwa Waendesha Bodaboda iliyofanyika kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga

MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akizungumza wakati wa halfa hiyo

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kulia akigawa riflect kwa Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Tanga katikati ni Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji na kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadat


MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kushoto akimkabidhi seti ya sofa msindi a Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi inayoendeshwa na Benki hiyo kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadat

Na Oscar Assenga, TANGA


BENKI ya CRDB imetangaza neema kwa wafanyabiashara wa bodaboda pamoja na bajaji kwamba hivi sasa hauitajiki kuwa na nyumba,gesti wala shamba kama dhamana ili kuweza kupata mkopo wa bodaboda.

Neema hiyo imetangazwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadat wakati wa halfa ya kugawa zawadi ya Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi iliyokwenda sambamba na ugawaji wa Riflect kwa Waendesha Bodaboda”,

Alisema kwamba wanachotakiwa ni kufika kwenye tawi lolote la benki hiyo na kumueleza Meneja wamefika kuchukukua bodaboda na dhamana yao na Bajaji ni ile kadi ya hicho kifaa.

Aidha alisema kwamba wameweza kutoa mikopo hiyo ili kuwaepusha wananchi na mikopo kausha damu na wamewapelekea riba nafuu sana kutokana na ombi la mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba.

“Bodaboda na waendesha bajaji wanasahauliwa sana lakini sisi kama benki ya CRDB tumeamua kuwawezesha wafanyabaishara wa bodaboda na bajaji hauitajiki kuwa na nyumba,sham,ba wale gesti “Alisema

Meneja huyo alisema kwamba benki hiyo wamejiwekea malengo ya kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi kwa kushirikiana na makundi yote ya wajasiriamali wakubwa,wa kati na wachini kabisa.

Alisema kwa sababu wanaamini kanzuri ya ijumaa inaandaliwa Alhamisi na wafanyabsiahara wakubwa wanaandaliwa tokea chini hivyo leo wanakwenda ramsi na mambo matatu ikiwa ni kutimiza agizo la RC Kindamba kushirikisha jamii ya wafanyabiashara wadogo wadogo katika suala la mitaji na biashara kwa ujumla.

Awali akizungumza katika halfa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba aliishukuru Benki hiyo kwa kuamua kuwezesha makundi hayo huku akitoa wito kwa watakao kupata mikopo wakaitumie kwa madhumuni yaliyokusudiwa ili waweze kufanya marejeshe kwa wakati.

Kindamba alisema kwamba pamoja na hayo lazima waendelee kutunza uaminifu ambao Benki ya CRDB wamewapa kwa kuhakikisha wanarejesha mkopo huo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kunufaika nao.

“Hasa wakina baba usije kupewa fedha ukaenda kuongea jiko watu wa Pwani tunajua wenyewe…fedha hiii ikatumike kwenye madhumuni yaliyokusudiwa”Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji  aliomba wafanyabiashara ndogo ndogo na maafisa usafirishaji
 waweze kutumia mikopo hiyo ili kuweza kujikwamua

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post