KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM CHAFANYIKA KISHAPU, VIJANA WATAKIWA KUTUMIA VIZURI UJANA WAO

Kikao cha Baraza la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kimefanyika leo Jumatatu Desemba 18,2023 kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ya kujenga umoja huo na Chama Cha Mapinduzi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili vijana.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa Mwanahalisa Daniel akitokea Mkoa wa Shinyanga amewataka vijana kuacha kuchezea ujana wao kwa kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa kama vile kukaa vijiweni lakini pia kuacha kukimbilia mikopo umiza maarufu Kausha damu mitaani ambayo imekuwa sio rafiki kwao na matokeo yake kuwarudisha nyuma kimaendeleo hivyo kuwakumbusha kufanya kazi wasitaka wapate pesa bila kutumia nguvu.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Benard Benson Werema amemshukuru Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaamini vijana na kuwateua katika nyanja mbalimbali za uongozi hali inayosaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana huku akiwataka vijana kujikita kufanya kazi wasisubiri teuzi kwamba zitawakuta wakiwa wanafanya kazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post