KAMPUNI YA ZAM SEED YAKABIDHI MSAADA WA MBEGU KWA WAKULIMA WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO

 


Ferdinand Shayo ,Manyara

Kampuni ya kuzalisha mbegu ya Zam Seed imetoa msaada wa tani 2 za mbegu za mahindi ili kuwasaidia wakulima walioathiriwa na mafuriko wilayani Hanang mkoani Manyara .


Akikabidhi msaada huo Meneja mauzo wa  Kampuni ya Zam Seed kanda ya kaskazini na kati Emanuel Mwakabana amesema kuwa msaada huo utawawezesha wakulima kurejea kwenye shughuli za kilimo na kupata chakula kipindi ambacho hali ya mvua imerejea katika hali ya kawaida.

Emanuel amesema kuwa kampuni ya Zam Seed imeamua kuungana na wakulima kuwapa pole kwa kukumbwa na janga la mafuriko kwa kuwapa mbegu hizo ambazo zinaweza kupandwa kwenye hekari 200.

"Palipo na mbegu pana matumaini hivyo msaada huu utarejesha matumaini kwa wakulima kuwa wanaweza kulima tena na kupata mazao "Afisa kilimo Halmashauri ya wilaya ya Hanang Samson Jeremiah ameipongeza kampuni ya Zam Seed kwa kuwa mstari wa mbele kuwasaidi wakulima ambao wapo katika wakati mgumu baada ya kupata mafuriko .

Pia amesema kuwa msaada huo utawanufaisha wakulima zaidia 200 waliothiriwa na mafuriko katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post