WAZIRI NDALICHAKO: TUTAENDELEA KUWAHUDUMIA WATANZANIA KWA UFANISI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,akizungumza kwenye kikao cha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Watumishi waliopo chini ya Ofisi yake kilichofanyika leo Novemba 11,2023 jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake zitaendelea kutekeleza majukumu kwa ufanisi na kuwahudumia wananchi kwa wakati.

Prof.Ndalichako ameyasema hayo Novemba 11, 2023 kwenye kikao cha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Watumishi waliopo chini ya Ofisi yake kilichofanyika katika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Ndalichako amesema katika kikao hicho kitawasaidia kukumbushana watumishi wajibu wao pamoja na kutengeneza ushirikiano na uhusiano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao.


“Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu tutaendelea kuwa timu imara ambayo lengo letu ni kuhakikisha kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zilizopo chini yake yatatekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post