WALIMU WA HESABU WANUFAIKA KATIKA MRADI WA MAFUNZO KAZINI


TAASISI za Vyuo Vikuu vya Elimu kutoka nchini Kenya,Zambia na Tanzania zimeshiriki semina iliyo andaliwa na mradi wa mafunzo kazini kwa walimu yenye lengo la kusaidia walimu wa sekondari wanao fundisha masomo ya hesabu ambapo itasaidia kuondoka changamoto ya somo la hesabu kwa Wanafunzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Nov 01,2023,Kaimu Mratibu Mradi Dkt.Perpetua Urio amesema Kuna mafunzo ambayo wakiyatumia yatasaidia kuwasaidia walimu waweze kuwa na kiwango cha kuwafundisha Vizuri na kuwasaidia Wanafunzi.

"Tulitumia ubunifu ambao wenzetu wa Elevetors Tanzania taasisi ambayo makao makuu yake yako huko Uswis walikua wameshaifanyia majaribio kwa Elimu ya msingi,Mradi wetu umedhaminiwa na IDRC na ilikua Mradi wa miaka miwili na nusu ambao tume utekeleza katika vyuo vikuu vya Elimu Kenya, Zambia na Tanzania,Mradi wetu umeshirikisha Wizara ya Elimu,Tamisemi,tumeshirikisha wadhibiti ubora, tumeshirikisha maafisa Elimu na afisa Elimu kata ambao wapo karibu kabisa na walimu"Amesema.

Aidha Dkt.Prpetua Amesema Uchache wa walimu wanao fundisha masomo ya hesabu ni sababu moja wapo inayo changia kuleta maumivu kwa watoto kutokana na mazingira anayo kuwa nayo mwalimu wakati wa ufundishaji hivyo kupelekea Wanafunzi kuchukia somo la hesabu.

"Walimu wahesabu unaweza kuta wapo wawili shule nzima kidato cha Cha kwanza hadi Cha sita anajiuliza kwanini mimi tu inapelekea mwalimu kukosa upendo kwa watoto hata watoto nao wakiona mwalimu Ana hasira wanaona hili Jambo no gumu"Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na ubunifu Prof.Aman Lusekelo kutoka chuo kikuu kishiriki Cha Elimu Dar Es Salaam(DUCE) amesema taasisi za Elimu zitumie utaalamu wao kutatu changamoto katika jamii na mradi umesaidia kwa upande wa walimu was masomo ya hesabu.

"sisi Kama chuo kikuu kishiriki tunasaidia na wanao andaa walimu mbinu nzuri za kufundisha hesabu Kama Mradi ingawa wanaonufaika kwa Sasa ni wachache haujafikia nchi nzima lengo la kuwaleta wakurugenzi wa Elimu maafisa Elimu,wapo wadhibiti ubora tutawaonesha picha na video,kwamba mbinu za kufundisha ni hizi huenda wakaona Mradi Sasa unafaa uwepo nchi nzima"Amesema

Naye Mhadhiri wa chuo kikuu Cha Dodoma Calvin Swai Amesema mradi una aksi malengo ya serikali na Wizara ya Elimu ya kutoa mafunzo kwa walimu kwani serikali imefanya makubwa kwa kuwapatia vishikwambi kwa kila mwalimu na kujikita kwenye mafunzo kwa walimu kila wiki.

"Tukiwa na miradi hii inakuja inaonesha tunashirikiana na serikali hivyo kuongeza nguvu,miradi Kama hii inahitajika zaidi tunapoelekea katika mtaalaa mpya na sera ya elimu Kuna mambo mapya ambayo na dhani ni muhimu kila mwalimu kuelewa mambo hayo na serikali iendelee kusaidia katika mambo haya"Amesema

Wanufaika wa mradi huo ni kutoka chuo kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam(DUCE),chuo cha Zambia,na Chuo Kikuu Cha Kenya na miongoni mwa walimu walio shiriki semina hiyo ni Kamisha wa Elimu,maafisa Elimu na maafisa Elimu Kata.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post