VIJANA WASISITIZWA KUZINGATIA MAADILI NA KUWA WAZALENDO


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza wakati akifungua kongamano la vijana la kisayansi lililofanyika Mkoani Morogoro.

Na; Mwandishi Wetu, MOROGORO

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewataka vijana nchini kuwa wazalendo na kuzingatia maadili ili kuwa taifa bora sasa na baadae.

Mhe. Katambi ametoa rai hiyo wakati akifungua kongamano la vijana la kisayansi lililofanyika Mkoani Morogoro kwa lengo la kujadili na kupata elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mapambano dhidi ya UKIMWI.

“Vijana wana mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa na wanaweza kutoa mchango mkubwa zaidi iwapo mtafanya shughuli zenu kwa kuzingatia uzalendo, weledi na maadili,” amesema.

Aidha, ameeleza kuwa Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI mwaka 2016/2017 nchini, umeonyesha kuwa moja ya makundi yaliyo nyuma katika kufikia malengo ni vijana huku wengi wenye umri mdogo hawajui hali zao za maambukizi ukilinganisha na watu wenye umri mkubwa, hali inayosababidha vijana wenye virusi vya UKIMWI kutoanza dawa za ARV mapema.

Vile vile, Mhe. Katambi ametoa rai kwa vijana nchini kujitokeze kwa wingi katika huduma za upimaji wa VVU kwa hiari sambamba na kupiga vita mmomonyoko wa maadili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post