UDOM YAJIDHATITI KUWA KITOVU CHA TEHAMA TANZANIA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka. 

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, amezindua Programu ya kuwajengea uwezo na kuendeleza ujuzi wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika masuala ya usalama wa mtandao katika chuo hicho ili kuendana na matakwa ya ulimwengu wa kidijitali. 

Akizungumza katika hafla hiyo November 10,2023 jijini hapa,Prof. Kusiluka, amesema kutokana na jinsi UDOM inavyofanya vizuri nchini na nje ya nchi kwenye masuala ya TEHAMA, kuna haja ya kuendeleza jitahada zaidi ili yoyote anayetamani kuwa mubobezi wa masuala ya TEHAMA chaguo lake  kuu liwe ni Chuo Kikuu cha Dodoma.

Pamoja na hayo amesema kuwa Chuo hicho(UDOM) kipo mbioni kuanzisha kituo atamizi cha TEHAMA ( Incubation Centre) kwa ajili ya kulea, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wanaosoma masuala ya TEHAMA na kukidhi mahitaji ya ulimwengu wa kidigitali. 

Naye Naibu Makamu  Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri kwa Umma, Prof. Razack Lokina, ameshukuru na kuipongeza Benki ya Stanbic kwa kuwezesha Programu hiyo na kusema  kuwa Stanbic imefanya chaguo sahihi kuanzisha programu hiyo UDOM. 

"Chuo chetu kipo vizuri,hamjakosea kuanza udhamini na wanafunzi wa UDOM, tupo vizuri kutokana na ubobevu tulionao katika ufundishaji masuala ya usalama wa mtandao na TEHAMA kiujumla, " amesisitiza Prf. Lokina. 

Akizungumzia namna Programu hiyo itakavyo wanufaisha Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma,Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia kutoka Benki ya Stanbic ambao ndiyo wadhamini Mussa Ally amesema kwa kuanza wataanza kwa kutoa  ufadhili kwa wahitimu 10 chuoni hapo.

"Tunanza na wanafunzi kumi wa UDOM waliofanya vizuri katika masuala ya usalama wa mtandao, kwa kuwatafutia vyuo ambavyo vitawapatia ujuzi zaidi na kuendeleza vipaji vyao kwa vitendo, sambamba na  kuwapatia ajira. Programı hiyo pia itahusika kuwatafutia fursa katika makampuni mengine Ulimwenguni, "amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post