SERIKALI YASEMA CHANGAMOTO YA UMEME NCHINI ITAKUWA HISTORIANaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Athumani Seleman wakati wa ziara ya kamati ya Kudumu ya bunge ya Nishati na madini kutembea vituo vya kuzalisha umeme vya Hale na Pangani Falls vilivyopo Mkoani Tanga

Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Nishati na madini David Mathayo akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Balozi Meja Jenerali Paul Sesa akizungumza wakati wa ziara hiyo

Na Oscar Assenga,KOROGWE

Serikali imesema kuwa mpaka ifikapo Mwezi Aprili mwakani changamoto ya uhaba wa umeme nchini itakuwa historia baada ya kumalizika Kwa ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme pamoja na bwawa la Nyerere linalotarajiwa kuzalisha zaidi ya Megga watts 200 ifikapo Januari mwakani.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya nishati Athumani Seleman wakati wa ziara ya kamati ya Kudumu ya bunge ya Nishati na madini kutembea vituo vya kuzalisha umeme vya Hale na Pangani Falls vilivyopo Mkoani Tanga.

Alisema kuwa tayari serikali imeweza kufanya uwekezaji mkubwa wa kukarabati vituo vya kuzalisha umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini ambapo utakapokamilika utasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme nchini.

"Hadi ifikapo mwezi Januari mwakani Bwawa la Nyerere litazalisha Kwa mara ya kwanza mega watts 235 ambapo itasaidia kupunguza upungufu wa mega watts 132 ambazo zitaweza kumalizwa mwezi wa pili Kwa kuongeza uzalishaji hadi kufikia mega watts 470"alisema Naibu Katibu Mkuu.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Nishati na madini David Mathayo aliitaka Wizara ya Nishati kuhakikisha miradi yote ya uboreshaji wa umeme inakamilika Kwa wakati na katika viwango bora

Alisema kuwa licha ya Miradi hiyo mingi kukamilika mwisho mwa mwezi Disemba mwaka 2025 lakini matarajio yetu ni kuona miradi hii inakamilika kabla ya muda Ili wananchi waweze kupata huduma

Dkt Mathayo alisema Serikali imewekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 50 katika mradi wa ukarabati wa kituo cha kuzalisha umeme cha Hale lengo ni kuhakikisha Umeme unapatikana

Alisema kutokana na uwekezaji huo wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuwekeza kwenye Umeme kiasi cha shilingi bilioni 50 ambazo zimetolewa kufanya matengenezo katika kituo hicho ambapo mradi ulioanza tangu mwezi Agosti 2023 na utakamilika Agosti 2025.

Hata hivyo alitumia ziara hiyo kulitaka Shirika la Umeme nchini Tanesco, Wizara ya Nishati na wakandarasi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Akiwa kwenye ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Balozi Meja Jenerali Paul Sesa amesema kuwa hali ya umeme imeimarika kwan hapo awali kulikua na upungufu wa Megawati 410.

Alisema lakini mpaka sasa upungufu wa Umeme umebaki megawati 120 na mpaka kufikia mwezi Aprili 2024hakutakua na upungufu wa Umeme.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post