MNADA WA CHAI KUKUZA NA KUENDELEZA ZAO LA CHAI NCHINI


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Hussen Omary amewaagiza wamiliki wa mashamba na viwanda vinavyochakata chai nchini kuzingatia malipo ya wafanyakazi wadogo katika viwanda hivyo ili kuendeleza zao la chai nchini.

Maagizo hayo ameyatoa leo katika hafla ya uzinduzi wa mnada wa zao la chai uliofanyika Dar es salaam wenye lengo la kukuza na kuendeleza zao la chai nchini ambapo Dkt Hussen ametumia hafla hiyo kueleza umuhimu wa mkulima mdogo katika kilimo hivyo ni budi kwa wamiliki wa mashamba kuzingatia masilahi ya wakulima hao.

Amesema hadi kufikia mwaka 2030 malengo ya Serikali ni kutengeneza ajira zaidi ya milioni tatu kupitia sekta ya kilimo ususani kwenye zao la chai

Imeelezwa kuwa kufanyika kwa mnada huo hapa nchini kutasaidia kuinua soko la chai ndani na nje ya mipaka.

Hivi ni mara ya kwanza kufanyika kwa mnada huo wa chai nchini ambapo unatajwa kusaidia kulitangaza zao la chai kwenye soko la nje.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post