KITANDULA ATOA MSAADA WA VYAKULA NA FEDHA KWA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO JIMBONI KWAKE


Na Mwandishi Wetu, MKINGA.

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ametoa msaada wa Vyakula na Fedha kwa Kaya 36 zilizopo kwenye Kata ya Manza na Mtimbwani wananchi katika Kijiji cha Msimbazi ambao walikumbwa na kadhia ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini

Kitandula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii aliamua kutoa msaada huo wakati akiwa kwenye ziara ya Jimbo hilo ili kuhakikisha wananchi hao wanaaondokana na changamoto ambazo wamekumbana nazo kutokana na uwepo wa mafuriko hayo

Akizungumza wakati akiwa kwenye ziara hiyo pamoja alipokwenda kushuhudia zoezi la ukoaji wa wananachi katika Kijiji cha Msimbazi Kata ya Manza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kitandula aliwaeleza wananchi hapo kwamba yupo pamoja nao na kuhaidia kuendelea kuwasaidia kuhakikisha wanaondokana na changamoto mbalimbali ili kuweza kujikwamua kiuchumi

Katika hatua nyengine Mbunge Kitandula alitoa msaada wa Pikipiki kwa kikundi cha wafugaji kwa ajili ya kukusanya maziwa kutoka kwa wafugaji wadogo wilayani humo.

Baada ya kuwakabidhi Pikipiki hiyo alimshukuru Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Maulid Surumbu kwa kumshirikisha kwenye jambo hili ni kazi kubwa na nzuri ambazo zimekuwa zikifanywa kwa ajili ya kuwakwamua kiuchumi wafugaji hao

“Nimeona niwaunge mkono kwa kuwapatia pikipiki hii naamini utakuwa chachu kwenu lakini pia niwaambie kwamba tupo pamoja na tutaendelea kushirikiana “Alisema

Awali akizungumza mmoja wa wanakikundi hao Abdala Mwajasi alimshukuru Mbunge huyo kwa msaada aliowasaidia huku akieleza mbunge huyo ni mahiri sana kuwasaidia wananchi hasa wanapokuwa wamekumbana na changamoto mbalimbali.

“Tunakushuru Mhe Mbunge Wetu kwa kutusaidia jambo hilo la umuhimu mkubwa kwa sababu sisi tauna uwezo wa kununua pikipiki “Alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post