UNESCO YAKABIDHI VIFAA VYA MAFUNZO YA MRADI WA BEAR II KWA MVTTC MOROGORO

SHIRIKA la Elimu , Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa mbalimbali vya mafunzo kupitia programu mpya ya mradi wa ‘Better Education for Africans Rise[BEAR II] kwa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro [MCVTTC].

Vifaa hivyo ni maalum katika Uandaaji na utoaji wa mafunzo ya Stashahada ya ufundi katika Sanaa za ubunifu na Kilimo-biashara [Creative arts and agri-business] vyenye thamani ya wastani wa Tsh 150,000,000 ambazo ni ufadhili wa ubia kati ya UNESCO na Jamhuri ya Watu wa Korea.

Awali akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Dar es salaam, Bw. Michel Toto ameshukuru kwa namna ya kipekee na heshima kubwa kwa waliofanikisha mradi huo kuanzia mwanzo ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Elimu pamoja na wadau wote.

‘’Katika muda mchache, wataalam hao wataonyesha utendaji kazi wa vifaa hivi vikiwemo vya usindikaji wa chakula na ufundi wa mikono vikiwemo Oveni ya gesi, Oveni ya kuokea ya umeme (vacuum oven, automatic gas oven, Electric baking oven & fermenting oven). Lakini pia vifaa vya mashine za kufunga maji na unga, kinu cha mahindi, kiuasha umeme wa jua na vingine vingi.

UNESCO inazingatia mpango wa Maendeleo endelevu wa [SDG 4], katika kutetea usawa na elimu bora ya ufundi na kuongezeka kwa idadi ya vijana na watu wazima wenye ujuzi wa kiufundi na ufundi kwa ajili ya ajira, kazi za staha na ujasiriamali, na kuondoa ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa taaluma.’’ Ameeleza Michel Toto.

Aidha, amesema Serikali na Chuo hicho kupitia mradi huo wa BEAR II, inaacha alama yake katika kushughulikia changamoto ya dunia ya kuhakikisha vijana wanawezeshwa kupitia elimu na kukuza ujuzi wao katika kukubiliana na soko la ajira.

Kwa upande wake,Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu, Dkt. Ethel Kasembe ameshukuru UNESCO na Watu wa Jamhuri ya Korea kwa msaada wa vifaa hivyo kwani vinaenda saidia ajira kwa Vijana na Watanzania kwa ujumla huku pia akipokea changamoto za Chuo hicho ikiwemo uchakavu wa majengo ambapo amesema wameichukua kuona namna ya kusaidia.

Nae Mkuu wa chuo hicho cha MVTTC, Samwel Kaali amepongeza UNESCO kwa vifaa hivyo huku wakiadi kuvitunza sambamba kuzalisha wataalam katika fani hizo mpya zitakazoanza chuoni hapo.

‘’Shukrani za dhati kwa UNESCO, VETA tutahakikisha vifaa hivi tunatunzwa vizuri ili vidumu na kuendelea kutumika kutolea mafunzi kwa muda mrefu zaidi.’’ Amesema Kaali.

Chuo hicho cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro[MVTTC] ni miongoni mwa Vyuo maalum vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi [VETA]ambapo kilianzishwa mwaka 1997 kupitia Sheria ya Bunge Na1 ya mwaka 1994 sura 82, marejeo ya mwaka 2019 pamoja na marekebisho yake mwaka 2021 na 2022 huku pia kikiwa na usajili wa Ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi [NACTVET] kikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya taaluma za elimu ya Ualimu wa Ufundi na Ufundi stadi pamoja na usimamizi wake.

Imeandaliwa na Andrew Chale, Morogoro-Mwandishi na Mpiga Picha.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Bw. Michel Toto akizungumza wakati wa tukio la kukabidhi vifaa vya mradi wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) wenye lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Shirika hilo na ubia wa pamoja na Jamhuri ya Watu wa Korea, tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Bw. Michel Toto akizungumza wakati wa tukio la kukabidhi vifaa vya mradi wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) wenye lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Shirika hilo na ubia wa pamoja na Jamhuri ya Watu wa Korea, tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu, Dkt. Ethel Kasembe akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vifaa wa mradi wa (BEAR II).Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro, Bw. Samwel Kaali,tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro, Bw. Samwel Kaali akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vifaa wa mradi wa (BEAR II).Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto na kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu, Dkt. Ethel Kasembe,tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto [kulia] wakiwa wameshika nyaraka ya makabidhiano ya vifaa hivyo na Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu, Dkt. Ethel Kasembe,tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Bw. Michel Toto akishuhudia vifaa hivyo wakati wa tukio la kukabidhi vifaa vya mradi wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) wenye lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Shirika hilo na ubia wa pamoja na Jamhuri ya Watu wa Korea, tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Bw. Michel Toto pamoja na mgeni rasmi wakipata maelezo ya vifaa hivyo namna vinavyofanya kazi wakati wa tukio la kukabidhi vifaa vya mradi wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) wenye lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Shirika hilo na ubia wa pamoja na Jamhuri ya Watu wa Korea, tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Bw. Michel Toto na mgeni rasmi na viongozi wengine wakionja mikate iliyotengenezwa na vifaa hivyo Chuoni hapo wakati wa tukio la kukabidhi vifaa vya mradi wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) wenye lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Shirika hilo na ubia wa pamoja na Jamhuri ya Watu wa Korea, tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto [kulia] wakiwa wameshika moja ya vifaa wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo na Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu, Dkt. Ethel Kasembe,tukio lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto [kulia] akiagana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu VETA, Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Bw. Felix Staki, Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu, Dkt. Ethel Kasembe na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro, Samwel Kaali wakati wa tukio kukabidhiwa vifaa lililofanyika katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post