TAKUKURU TANGA YABAINI MAPUNGUFU UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO YA BILION 5

Afisa Uchunguzi Mwandamizi TAKUKURU mkoa wa Tanga Frank Mapunda

Na Pamela Chaula - Tanga

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  mkoa wa  Tanga  kwa kipindi cha  Julai hadi Septemba 2023 imefuatilia utekelezaji wa miradi 60 yenye thamani ya sh 10,621,271,204.00/=  na miradi 28 yenye thamani ya sh 5, 072,000,000.00/=  ilibainika kuwa na mapungufu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Afisa Uchunguzi Mwandamizi TAKUKURU mkoa wa Tanga Frank Mapunda ameeleza mikakati na mafanikio yaliyopata kwa miezi mitatu kwa kushirikiana na wadau  katika utekelezaji wa miradi ya BOOST.

Mapunda amesema kuwa vikao vilivyofanyika mwanzoni mwa miradi Boost vimesaidia kuziba mianya ya rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Tanga.

Katika utekelezaji wa majukumu ya uzuiaji na kupambana Rushwa Mapunda amesema Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga imefanikiwa kufanya uchambuzi wa mifumo Tisa (9) ili kuleta tija na mifumo imara isiyokwamisha utoaji wa huduma Bora kwa wananchi .

Aidha Taasisi hiyo kwa  kushirikiana na wadau  imepokea taarifa 142 ambapo taarifa 89 ni vitendo vya Rushwa na taarifa 53 si za vitendo vya rushwa na mashauri saba (7) mapya yamefunguliwa mashtaka Hadi Sasa Jamuhuri imeshinda shauri 1 na 26 yanaendelea mahakamani.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post