MBUNGE WAITARA AGAWA MAJIKO 200 YA GESI KWA WANANCHI WA TARIME VIJIJINI


Na Deborah Munisi - Tarime

Katika kukabiliana na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi hapa nchini Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mhe. Mwita Waitara amegawa majiko 200 kwa wananchi wa Jimbo hilo huku dhima kuu ikiwa ni kupunguza matumizi ya nishati ya Mkaa na Kuni kwa wananchi.


Ugawaji huo wa gesi umefanyika Novemba 23, 2023 katika hafla ya chakula cha pamoja iliyohudhuriwa na viongozi wa CCM wa kata zote za Jimbo la Tarime vijijini, viongozi wa jumuiya UWT kata zote na wawakilishi wa vikundi kutoka kata zote iliyoandaliwa na Mbunge huyo nyumbani kwake katika kata ya Itiryo Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Majiko hayo wamepewa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata zote jimboni humo, viongozi wa Jumuiya ya Wanawake, vikundi vya wanawake na vijana wajasiriamali vilivyosajiliwa chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Mbunge Waitara amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu Jimboni kwake kwani kufanya hivyo itakuwa ni mwarobaini wa kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.


Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe. Patrick Chandi na wajumbe wa kamati ya siasa mkoa na Wilaya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post