WAAJIRI WA MAKAMPUNI SEKTA YA UJENZI WAPATIWA ELIMU KUHUSU SHERIA ZA KAZI

 


Na Mwandishi Wetu; Dodoma
 
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyenye Ulemavu pamoja na Taasisi zake imetoa elimu ya Sheria za Kazi kwa waajiri wa makampuni ya sekta ya ujenzi ili kuwajengea uelewa wa kuwa na mikakati ya kutekeleza na kuzingatia matakwa ya Sheria za Kazi katika sehemu za kazi.
 
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 1 Novemba, 2023 jijini Dodoma Kamishana wa Kazi Msaidizi wa Vibali vya Kazi, Lilian Francis amesema kwamba pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kusimamia utekelezaji wa sheria katika Sekta ya Ujenzi kumekuwa na changamoto hususan katika masuala ya viwango vya Kazi.
 
Aidha amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Taasisi zilizopo chini yake ikiwemo OSHA, WCF na NSSF imeona umuhimu wa kutoa Elimu ya Sheria za Kazi kwa Waajiri ili kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima sehemu za kazi.
 
Ameongeza kuwa kikao hicho ni muhimu kwa ustawi wa Waajiri na Wafanyakazi waliopo katika Sekta ya Ujenzi na kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla pamoja, pia kuhakikisha haki na maslahi ya pande zote yanazingatiwa ipasavyo.
 
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine Mkurugenzi wa Sheria wa Kampuni ya Mohammedi Builders Bw. Nixon Tagara amesema Elimu hiyo waliyoipata itawasaidia kuongeza uelewa kuhusu haki ya mfanyakazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post