WATALAKA NA WATALAKIWA WAPEWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 



MKUU wa Idara ya Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Tanga Sharifa Coshuma akizungumza wakati akifungua mafunzo ya watalaka na watalakiwa yaliandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR)yaliyolenga kutoa elimu kwa kundi hilo la watalaka na watalakiwa ya ujasiriamali kwa lengo ka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirika hilo Lulu George na kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Rodgers Chamani


MKUU wa Idara ya Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Tanga Sharifa Coshuma akizungumza wakati akifungua mafunzo ya watalaka na watalakiwa yaliandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR)yaliyolenga kutoa elimu kwa kundi hilo la watalaka na watalakiwa ya ujasiriamali kwa lengo ka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kushoto


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR) Rodgers Chamani akizungumza wakati wa mafunzo hayo kulia ni Katibu wa shirika hilo Lulu George

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR) Rodgers Chamani  akizungumza wakati wa mafunzo 

Katibu Mkuu wa Shirika hilo Lulu George akisisitiza jambo wakati akitoa mada katika mafunzo hayo



Afisa Miradi wa Shirika hilo Sadick Shembilu akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo

Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi




Na Oscar Assenga, TANGA

MKUU wa Idara ya Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Tanga Sharifa Coshuma  amefungua mafunzo ya watalaka na watalakiwa huku akifichua siri ya wanawake wengi kuishi marefu kuliko wanaume kwamba ni uvumilifu na kutoishi na viny’ongo moyoni.

Mafunzo yaliandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Msamaria Mwema (Good Samaritan Charitable and Pain Relief-GSCPR)yaliyolenga kutoa elimu kwa kundi hilo la watalaka na watalakiwa ya ujasiriamali kwa lengo ka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Sharifa alisema Wanawake wengi ni wepesi kuzungumzia matatizo yao tofauti na wanaume hatua inayowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo na kuweza kuishi kwa muda mrefu bila chuki wala vikwazo.

“Kwa kweli kuzungumza na kuwa wawazi ndio tiba sahihi katika jambo lolote katika kumuweka mtu huru lakini viny’ongo havisaidii na vinakuwa vibaya sana katika jamii na hatarishi kwa afya“,Alisema Afisa huyo.

Aliwataka wanawake hao kuzingatia mafunzo wanayopewa kwa mustakabali wa maisha yao na familia hasa kwa kuzungitia kuwa jukumu la malezi ya watoto bado lipo mikononi mwao


Awali akizungumza katika mafunzo hayo Katibu Mkuu wa Shirika hilo Lulu George alianza kuwashukuru TPA kwa kuwapa nafasi ya kushirikiana na wakina mama hao ili kuwawezesha kupata mafunzo ya kujikomboa kiuchumi.

Lulu alisema wanaamini kama taassi mbalimbali zilizopo Mkoani Tanga zikiendelea kuwashikia mkono itawezesha Shirika hilo kusambaza elimu ya ujasiriamali,kujitambua,maisha baada ya talaka sambamba na changamoto ya ukomo wa hedhi kwenye makundi mbalimbali kwa jamii.

“Tunaamini wakina mama hao wakiwa na akili iliyotulia wanaweza kufanya mabadiliko mazuri ya kiuchumi,kupitia wamama hawa hawa wataweza kuitumia Bandari yetu ya Tanga kufungua fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi na hatimaye kuongeza pato la mtu mmoja mmoja,mkoa na Taifa kwa ujumla”,alifafanua.

Katibu Mkuu huyo alisema baada ya mafunzo hayo wanatarajia kuunda vikundi vitakavyowezesha wamama hao kufanya shughuli zao kwa pamoja na hatimaye kufikia malengo waliyokuwa wamejiwekea katika kukidhi mahitaji yao.

“Yapo mambo mengi wanaweza kufanya kwani Mkonge peke yake wakitumia fursa iliyopo katika kuongeza thamani kwa bidhaa zinazotokana na zao hilo watafika mbali kwa sababu uhitaji wa bidhaa za zao la Mkonge ndani na nje ya nchi bado ni mkubwa sana ,tunatarajia wamama hawa wafike kwenye soko la dunia”,alisema.

Hata hivyo aliisihi jamii kuondoa dhana kwamba mtu aliyetalakiwa ni mtu mwenye laana au aibu kwani unyanyapaa huo husababisha watu waliotalikiana kuishi katika maumivu makubwa na kushindwa kujisamehe.

“Lakini tuwashukuru Bandari ya Tanga kwa kuwaezesha kuendelea kuwapa matumaini kundi hili ambalo kwenye jamii lilionekana kwamba mtu akipewa talaka amelaaniwa au hafai lakini mara baada ya kuwapa mafunzo kuna maisha baada ya talaka wakina mama hawa wamekuwa watulivu na wameweza kurudisha tabasamu la matumaini”alisema.

Lulu alisema Shirika la Msamaria Mwema linaendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kumkomboa mwanamke kwenye nyanja zote ikiwa ni pamoja na kulinda afya ya akili changamoto inayowakabili wanawake wengi kwa sasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post