TUTAFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO KWA MASLAHI YA VIJANA WOTE NCHINI - CDE LULANDALA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC),akizungumza na Vijana wote nchini kupitia mkutano maalum uliofanyika katika tarehe 20 Oktoba, 2023 Viwanja vya Vijana Social Kinondoni Dar es Salaam .

......................

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amezungumza na Vijana wote nchini kupitia mkutano maalum uliofanyika katika tarehe 20 Oktoba, 2023 Viwanja vya Vijana Social Kinondoni Dar es Salaam .

Lengo la mkutano huo ilikua Mwenyekiti Ndugu Kawaida kutoa maelekezo Mahsusi ya kiutendaji kwa Katibu Mkuu wa Jymuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Malinduzi Komredi Fakii Raphael Lulandala (MNEC) na Viongozi wote wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Nchini.

Mkutano huo umehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti UVCCM Komredi Rehema Sombi Omary (MNEC) Katibu Mkuu UVCCM Komredi Fakii Raphael Lulandala (MNEC) , Wakuu wa Idara za UVCCM Taifa na Watendaji wa Jumuiya kutoka Mikoa yote nchini, Baadhi ya Wenyeviti wa Jumuiya kutoka Mikoa jirani, na Maelfu ya Wanachama kutoka Mkoa wa Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post