TTB YASHINDA TENA KUWA BODI BORA YA UTALII BARANI AFRIKA

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko , Dkt. Gladstone Mlay akitoa taarifa ya ushindi wa Tanzania wakati wa mkutano na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

******************

Bodi ya utalii Tanzania (TTB) imeshinda tuzo ya WORLD TRAVEL AWARDS 2023 na kuwa Bodi Bora ua Utalii Afrika baada ya kushindanishwa na bodi nyingine za nchi za Afrika. Hii ni mara ya pili ya mfululizo kwa TTB kushinda tuzo hiyo katika kipengele cha bodi bora ya utalii Afrika.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Dkt. Gladstone Mlay kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliyofanyika Oktoba 17, 2023 jijini Dar es salaam, wenye lengo la kuuhabarisha umma kuhusu ushindi wa Tanzania katika mashindano hayo yanayoandaliwa na kampuni ya World Media and Events Limited ya nchini Uingereza.

Dkt. Mlay amesema kuwa Tanzania imeweza kuibuka kidedea kwenye vipengele vingine mbalimbali ambapo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imekuwa hifadhi bora barani Afrika kwa miaka mitano (5) Mfululizo na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro limeshinda katika kipengele cha kuwa Kivutio bora barani Afrika.

Vivutio hivi vimeweza kupata kura nyingi kutokana na Juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuvitangaza kupitia filamu ya Tanzania: The Royal Tour yenye mchango mkubwa wa kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania inatoa pongezi kwa wadau wote wa utalii waliyoshiriki katika mashindano ya World Travel Awards 2023 na kufanikiwa kushinda katika vipengere tofauti ambapo amezitaja kampuni zilizoshinda ni; Zara Tours, Thanda Island, Zanzibar Serena Hotel, Gran Meliá Arusha, First Car Rental Tanzania, Green Inspirations DMC, Auric Air, Gran Meliá Arusha,

Kampuni nyingine zilizoshinda ni Meliá Zanzibar, Twiga Tours, Lamai Serengeti, Kuro Tarangire, Satguru Travel Tanzania, FCM Travel - Tanzania (Skylink Travel & Tours), Qambani, ZanTours, Park Hyatt Zanzibar, Meliá Zanzibar, Gosheni Safaris.

Kwa upande wa Afisa Masoko wa Kampuni ya Zara Tours, Bi Nancy ngotea aliyepata kuwa mwakilishi wa wadau wa utalii katika mkutano huo, ametoa rai kwa wadau wote wa Utalii kutumia fursa ya mashindano haya kama njia ya kutangaza kampuni zao katika masoko ya utalii ya kimataifa.

Mashindano ya World travel Award hufanyika kila mwaka, ambapo washindi wanapatikana kwa njia ya kupigiwa kura kupitia tovuti ya kampuni hiyo.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Zara Tours , Bi. Nancy Ngatea akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post