TOIO WAJA NA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE VYOMBO VYA MOTO VISIVYOTUMIA MAFUTA

Na Oscar Assenga,TANGATAASISI ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) wameamua kutumia Uchumi wa Buluu kwa kutengeneza vifaa vya moto ambavyo havitumii mfumo wa mafuta kwa kuanzisha kiwanda kidogo ambacho kitakuwa kinaviunda


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organisation(TOIO) Shaukatali Hussein wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kiwanda hicho kidogo kitatoa fursa kwa vijana na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kufundishwa jinsi ya kutengeneza na kuviunda.


Alisema watafundishwa namna ya kuunda pikipiki za kawaida na zile za magurudum matatu maarufu bajaji za umeme ambazo inatajwa zitakuwa kimbilio la wananchi kutokana na gharama za mafuta kupaa juu kila wakati.


“Mkakati wa kuunda kiwanda cha kutengeneza magari ya kutumia umeme bado hawajafikia hatua hiyo kutokana na kwamba hivi sasa wapo kwenye mafunzo mwakani wanatarajia kupata nafasi kubwa kutoka Halmashauri wataweka nguvu kubwa kwenye kiwanda rasmi cha mafunzo na kuunda vyombo hivyo”Alisema


Hussein alisema kwamba licha ya wao kuendelea kutoa ujuzi huo na mafunzo kwa vijana bure lakini mwitikio wao bado upo chini hivyo wanawataka wao namna ya kuchangamkia fursa hizo ili baadae waweze kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao.


Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyo alisema Serikali imejitahidi sana kuwasaidia na wamepata msaada mkubwa lakini kikubwa ni kuona namna ya kubadilisha mawazo na mtazamo wa vijana kuweza kuchangamkia fursa ya kujiunga kwenye mafuinzo ya uundaji wa vifaa hivyo


Kuhusu leseni wakati wakipata kuunza vifaa hivyo lazima uwe na leseni au kibali hivi sasa wamezungumza na Mkurugenzi wa Jiji na RC wapo kwenye mchakato wa kufanya maandalizi ya kupata leseni ili vifaa vikija wavitapate kwa bei nafuu na vijana kuweza kuvipata .


Hata hivyo alisema wamefanya mazungumzo na vijana ikiwemo Benki ya CRDB kuvipatia vikundi vya vijana mikopo kwa bei nafuu wanaomba wakishapata leseni na kiwanda kila kitu kitakuwa vizuri.


Awali akizungumza mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Tanga Ufundi anayepata mafunzo hayo Castro Molel alisema mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwao na kuweza kuwaongezea ujuzi.


Alisema hivi sasa wametengeneza mfumo ambao mgonjwa anaweza kupata huduma ya daktari akiwa nyumbani bila kuwa na usumbufu wa kwenda hospitali.


Molel alisema ni kama mfumo wa kufanya mazungumzo na daktari kwamba kuna siku utakwenda kupata huduma hivyo siku akiwa na nafasi anampa majibu na hivyo naye kwenda kupata matibabu


Alisema kupitia mfumo huo unaingia kwenye mtandao na unatengeneza akaunti na unaweza kuona orodha ya madaktari waliopo na kuweza kumchagua na kuweza kuwasiliana naye na kuomba huduma kjama kuna nafasi unakwenda kuonana naye bila usumbufu.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organisation(TOIO) Shaukatali Hussein akizungumza na waandishi wa habari 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organisation(TOIO) Shaukatali Hussein akimuonyesha mwandishi wa habari wa ITV William Mngazija vitu mbalimbali walivyoviunda
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organisation(TOIO) Shaukatali Hussein akimuonyesha mwandishi wa habari wa ITV William Mngazija vitu mbalimbali walivyoviunda

 mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Tanga Ufundi anayepata mafunzo hayo Castro Molel  akielezea manufaa ya mafunzo hayo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post