RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA NCHINI INDIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023. Rais Samia ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho nchini India. Ni Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post