MHANDISI LUHEMEJA ATAKA WCF KUSAJILI WAAJIRI WOTE NCHINI

 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  wilayani Morogoro.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akisisitiza jambo kwenye kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  wilayani Morogoro.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt.John Mduma akizungumza kwenye kikao hicho Oktoba 19, 2023 wilayani Morogoro

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakimsikiliza Katibu Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja kwenye kikao cha Baraza hilo wilayani Morogoro.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wilayani Morogoro.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa maagizo manne kwa Baraza la wafanyakazi la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ikiwamo kuwasajili waajiri wote nchini.

Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo  wilayani Morogoro alipokuwa akifungua kikao cha Baraza hilo.

Amesema ni muhimu WCF ikaongeza malengo ya kusajili waajiri wote hasa wa sekta binafsi ambao wanaajiri wafanyakazi wengi wa ngazi ya chini na wanaofanya kazi kwenye mazingira hatarishi.

“Suala jingine ni elimu kwa umma huu mfuko ni muhimu unawagusa watanzania wote kutokana na wapendwa wao kupata madhira kazini, wajue manufaa ya mfuko na majukumu yake,”amesema.

Pia, amehimiza kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ili watanzania wavutiwe na huduma zinazotolewa.

“Mmbebe jukumu hili kwa pamoja na kazi hii muibebe kwa moyo lakini mkifanyia kwa maslahi hamtafanikiwa, pia suala jingine ni mashirikiano fanyeni kazi kama timu muheshimiane wafanyakazi na viongozi ili kuleta ufanisi wa mfuko,”amesema.

Naye, Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, amesema mfuko upo imara na wajumbe wa baraza hilo wamejadili masuala mbalimbali ikiwamo huduma za utengamao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post