IHEFU FC YAICHAKAZA YANGA.....YAIDUNGUA 2-1Timu ya Yanga Sc imepokea kichapo cha goli 2 - 1 kutoka kwa Ihefu Fc.

Mchezo huo umepigwa leo Oktoba 4, 2023 katika uwanja wa Ubaruku ulioko Mbalali jijini Mbeya.

Ambapo katika mchezo huo uliomalizika kwa dakika 90 na kuwaacha mashabiki wa timu ya Yanga sc midomo wazi wakishuhudia timu yao ikipoteza kwa kichapo cha goli 2 dhidi ya Ihefu Fc.

Goli la kwanza likifungwa na Professor Pacom Dakika ya 3 huku magoli ya Ihefu Fc yakifungwa na wachezaji Kisu Dakika ya 40 na goli la pili likifungwa na Ilanifya dakika ya 67 ya mchezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post