WATU 2,600 WATIBIWA MACHO BUGANDO KILA MWEZI


Mkuu wa Idara ya Macho Bugando, Dk Christopher Mwanansao akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Macho duniani yaliyofanyika kikanda katika viwanja vya hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Macho Bugando, Dk Christopher Mwanansao akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Macho duniani yaliyofanyika kikanda katika viwanja vya hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dk Fabian Massaga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika katika maadhimisho ya Siku ya macho Duniani yaliyofanyika kikanda katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dk Fabian Massaga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika katika maadhimisho ya Siku ya macho Duniani yaliyofanyika kikanda katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza

****
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imesema wastani wa watu 2,600 hutibiwa maradhi ya macho hospitalini hapo kila mwezi.

Taarifa hiyo ilitolewa leo na Mkuu wa Idara ya Macho Bugando, Dk Christopher Mwanansao wakati wa maadhimisho ya siku ya macho duniani iliyoadhimishwa kikanda katika viwanja vya hospitali hiyo ikitanguliwa na uchunguzi wa maradhi ya macho kwa wananchi.

Dk Mwanansao amesema wagonjwa wengi wanaohudumiwa katika kliniki ya Bugando hukutwa na tatizo la saratani ya mtoto wa jicho,  mzio wa macho, presha ya macho, kisukari cha macho na huoni hafifu, ambapo asilimia 60 ya watu wanaopata upofu hutokana na tatizo la mtoto wa jicho ambalo huwakumba zaidi wazee na watoto.
 
"Kliniki yetu baada ya kuboreshwa tumekuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa takribani 100 kwa siku, 500 kwa wiki na 2,400 mpaka 2,600 kwa mwezi na visababishi vikubwa vya magonjwa ya macho ni umri, mazingira yanapelekea kupata mzio kwenye macho, kurithi, kisukari na presha pia hupelekea kupata magonjwa ya macho," amesema Dk Mwanansao


Amesema "Kwa sehemu kubwa matatizo ya macho yanasababishwa na umri unapoenda ndipo watu wengi wanapata matatizo hayo, hivyo, unapofikisha miaka 40 walau uende hospitali kuchunguza uwezo wako wa kuona. Pia watoto wengi wanazaliwa na mtoto wa jicho kutokana na maambukizi ya mama, magonjwa ya kurithi na kisukari,"


Amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi na vipimo vya macho mara kwa mara ama angalau mara mbili kwa mwaka ili kuimarisha uoni wao na afya ya macho yao.

"Kuna haja ya kupima macho hata kama hayana tatizo kwa mfanonpresha ya macho katika hatua za awali huwa haina dalili, kwahiyo unaanza kupoteza uoni pembeni. Watu wapende kwenda kupima macho na wachukue hatua mbalimbali za kukinga macho mapema," amesema Dk Mwanansao


Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Fabian Massaga alisema hospitali inafanya jitihada kuhakikisha hakuna mwanachi anayepoteza uoni kwa changamoto za macho kwa kuboresha miundombinu, kutoa huduma za kibingwa katika hospitali za wilaya na mikoa, kutoa huduma za upasuaji kwa gharama nafuu na vipimo vya bure.


"Sisi hospitali ya Bugando tunaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu ili wananchi wa Kanda ya ziwa muweze kunufaika na huduma zetu," amesema Dk Masaga

Suzan Steven mkazi wa Bariadi mkoani Simiyu, alisema akiwa anafanya kazi ya katibu muhtasi alianza kusumbuliwa na macho na kuamua kuacha kazi sasa ni mwaka wa tatu na ameamua kufika Bugando kupata matibabu.



Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Dk Fabian Massaga (suti nyeusi) akisalimiana na wananchi waliofika katika maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya macho duniani yaliyofanyika hospitalini hapo leo Oktoba 12,2023. Aliyesimama kulia ni Mkuu wa Idara ya Macho Bugando, Dk Christopher Mwanansao.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Dk Fabian Massaga (suti nyeusi) akisalimiana na wananchi waliofika katika maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya macho duniani yaliyofanyika hospitalini hapo leo Oktoba 12,2023. Aliyesimama kulia ni Mkuu wa Idara ya Macho Bugando, Dk Christopher Mwanansao.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dk Fabian Massaga (suti nyeusi katikati) akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bugando na watumishi wa Idara ya Macho Bugando baada ya maadhimisho ya Siku ya Macho yaliyofanyika kikanda katika viwanja vya hospitali hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post