KANISA LA WASABATO LUBAGA LAENDESHA HARAMBEE UJENZI WA GHOROFA 'KIBWETA' .... DC SAMIZI ATAKA VIONGOZI WA DINI KUIMARISHA USIMAMIZI MALEZI YA WATOTO

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wa tatu kutoka kushoto Johari Samizi akiongozana na Mgeni Rasmi kuelekea Kanisani kwa ajili ya Shughuli ya harambee ya ujenzi wa Kibweta katika kanisa la Wasabato Lubaga.

NA MWANDISHI WETU-SHINYANGA.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh.Johari  Samizi amewaomba viongozi wa dini Wilayani huko  kuimairisha na kusimamia malezi kwa Watoto na jamii  ili kuwa na taifa na waumini wenye hofu ya Mungu ambao watachangia kuendeleza taifa kwa kuwa lilipo fika ni uwepo wa kazi kubwa ya watumishi wa Mungu.

Samizi ameleeza hayo leo Jumamosi Oktoba 28,2023 wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Wadventista Wasabato Lubaga katika ibada  maalumu ya harambee kwa ajili ya ujenzi wa kibweta cha Ghorofa tatu  katika kanisa hilo kitakachokuwa na Shughuli mbalimbali.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wa pili kutoka kulia  Johari Samizi akiwa na Mgeni Rasmi  wakati wakipokea salutiuelekea Kanisani kwa ajili ya Shughuli ya harambee ya ujenzi wa Kibweta katika kanisa la Wasabato Lubaga.Baadhi ya Vijana wa Kanisa hilo wakionyesha ishara ya ukakamavu mbele ya mgeni rasmi.Mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa kibweta katika kanisa la waadvenstista wasabato Lubaga Nehemia Makindo akieleza nafasi na umuhimu wa kuchangia masuala ya kikanisa ambapo amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 10 pamoja na mifuko ya saruji mia 500.

Samizi amesema Serikali inatambua  na kuheshimu mchango mkubwa unaotolewa na viongozi wa dini katika kukuza na kutunza amani na mshikamano wa nchi,hali ambayo imechangia kuendelea kwa utulivu nchini ambapo amewataka kuendelea kuwakumbusha waumini wao wajibu wa kuwa na hofu ya Mungu.

Aidha Samizi amesema kumekuwapo na Mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa jamii ambao unachangiwa na wazazi kutokuwa na muda wa kutekeleza majukumu yao iapsavyo ya malezi kwa kuwandaa Watoto kuwa wzazi bora wa kesho  na kuwa bize shughuli za Maisha na kusaka uchumi na kusahau malezi ya Watoto.

Samizi ameongeza kwa kusema kuwa wazazi na jamii wanalojukumu kubwa la kuhakikisha wanalea Watoto katika msitari ulionyoka ili kuwa na jamii, waumini na taifa lenye kumtukuza  Mungu na kuwa na hofu pia.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amesema halmashauri ya Manispa ya Shinyanga kazi yake kubwa ni kutoa huduma kwa jamii ambapo amesema kanisa ni sehemu kubwa ya utekelezaji wa miradi ya  kwa kuiasa jamii kuishi na kutenda katika usawa.

Masumbuko amesema Viongozi wa Kiroho  wana mchango kubwa katika maendeleo ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuelekeza, kufundisha na kuongoza waumini wao hali inayofanya suala la utekelezaji wa miradi linakwensa pasipo kuwa na hofu.

Wakati huo Masumbuko amesema kila mmoja ana wajibu wa kutimiza malengo yake ili kuhakikisha jamii inaishi vema.

Mgeni rasmi katika harambee hiyo ya ujenzi wa Kibweta katika kanisa hilo Nehemia Makindo amesema kuwa jukumu la kujenga kanisa au nyumba ya Mungu ni la kila muumini hivyo ni wajibu wao kulijenga kanisa.

Nehemia ameongeza kuwa pasipo kuijenga nyumba ya Mungu ni kazi bure hivyo wao kama waumini wanapswa kusimama katika kujenga na kuimairisha eneo la kuabudia ili waumini waweze kupata huduma za kiroho katika eneo lenye amani.

Mchungaji aliyeongoza ibada ya harambee hiyo, Reward Mmbaga amewataka watanzania na waumini kujenga utaratibu wa kutoa kwa kuwa kutoa kuna nguvu kubwa ndani yake. (Luka 6:38).

Amesema kujenga utaratibu wa kutoa kuna nguvu kubwa na kiwango kikibwa hivyo ni vema wauimini wakaujenga mfumo  huo na kuwafundisha Watoto wangali wadogo

Ujenzi wa Kibweta hicho chenye Mimbari ya Kisasa,Kisima cha ubatizo,Sehemu ya kubadili nguo kwa wabatizwa,Ofisi za Idara,Ofisi za Wazee wa Kanisa,Ofisi ya Mchungaji,Ukumbi wa Mikutano,Studio ya Kisasa na Hosteli inataji kugharimu shilingi Milioni mia sita hadi kukamilika kwake(600,000,000.) ambapo ujenzi huo umegawanyika katika awamu tatu.

Aidha awamu ya kwanza ujenzi unataraji kugahrimu milioni 150 ikiwa ni ujenzi wa Msingi na Kunyanyua nguzo,awamu ya pili milioni 150 ikiwa ni ujenzi wa ghorofa ya kwanza nay a pili huku awamu  ya tatu ikigharimu milioni 300 kwa ajili ghorofa ya tatu,kuezeka,miundombinu na umaliziaji.

Katika harambee hiyo iliyofanyika leo October 28, 2023 katika kanisa la wadventista wasabato Lubaga jumla ya milioni 113,678,600 zimepatikana ikiwa keshi ni Milioni 56,446,100 huku ahadi ikiwa ni milioni 57,232,500.

Aidha jumla ya mifuko ya saruji 660 imepatikana katika harambee hiyo, Mchanga tripu 34, Nondo 5 na Ng’ombe mmoja ikiwa ni sehemu ya harambee hiyo ili kufikisha milioni 150 zinazohitajika katika ujenzi wa awali wa Msingi na Nguzo za jengo hilo.

Baadhi ya Vijana wa Kanisa hilo wakionyesha ishara ya ukakamvu mbele ya mgeni rasmi.

Mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa Kibweta cha kanisa la wasabato Lubaga Ndugu Nehemia Makindo akisaini kitabu cha wageni.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akisaini kitabu cha wageni katika harambee ya ujenzi wa kibweta cha Kanisa hilo.
Mwonekano wa Jengo la Kibweta cha Ghorofa tatu litakalojengwa katika kanisa la SDA Lubaga Shinyanga.
Viongozi wakiendelea kupata maelezo ya namna ujenzi huo utakavyokuwa na kugharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 600.
Kwaya ikiimba katika harambee hiyo October 28,2023.
Wa kwanza kushoto ni diwani wa kata ya Ngokolo Victor Mkwizu,akiwa na viongozi wengine katika ibada ya harambee ya ujenzi wa kibweta cha ghorofa tatu kanisa la SDA Lubaga.
Kwaya ya Maranatha kanisa la SDA Lubaga wakiimba kwenye harambee ya ujenzi wa kibweta cha ghorofa tatu October 28,2023. 


Mchungaji akiendesha sala fupi kwa ajili ya maandalio ya ibada ya harambee kanisa la SDA Lubaga. 
Waumini wakiendelea na maombi.

Mwakilishi wa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga akieleza mchango wao katika ujenzi huo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mh.Elias Masumbuko akizungumza katika harambee ya kuchangia kujenga kibweta cha Kanisa la SDA Lubaga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Joahri Samizi akizungumza katika harambee ya kuchangia kujenga kibweta cha Kanisa la SDA Lubaga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiteta jambo na Mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa Kibweta Ndugu Nehemia Makindo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiteta jambo na Mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa Kibweta Ndugu Nehemia Makindo pamoja na Mwekezaji Mzawa Ndugu Giritu Makula.
Mchungaji Reward Mmbaga akiongoza neno la siku katika harambee ya ujenzi wa Kibweta cha Ghorofa tatu kwa ajili ya kumtukuza Mungu.Baaadhi ya Viongozi wa Kanisa la Wadventista Wasabato Lubaga wakiwa wameketi.

Fadhil Tawei akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa tatu litakalojengwa katika Kanisa la SDA Lubaga-Shinyanga

 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akitoa ahadi ya Milioni moja katika kuchangia ujenzi wa kibweta cha ghorofa tatu SDA Lubaga. 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mh.Elias Masumbuko akiahidi kutoa milioni moja kuchangia ujenzi huo.
Diwani wa kata ya Ngokolo Victor Mkwizu akitoa ahadi kwa waumini wa SDA Lubaga.
Mkurugenzi wa Giritu Interprises Giritu Makula akitoa mchango wake wa shilingi Milioni 3 katika kuchangia ujenzi huo wa kibweta SDA Lubaga.

Mmoja wa Wazee wa Kanisa la SDA Lubaga-Shinyanga 
Mzee wa kanisa la SDA Lubaga Mr. Wembe akitoa mchango wake wa milioni 2 kwa ajili ya ujenzi.

Zoezi la uchangiaji ujenzi likiendelea katika kuhakikisha linafanikiwa
-- 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post