MUWAACHE WANANGU WASOME NITAWAFUNGA MIAKA 30 JELA : RC DKT. NAWANDA
Maswa,

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Nawanda amewaasa Vijana Wilayani Maswa kuacha tabia ya kujihusisha  kimapenzi na Wanafunzi na badala yake wawaache watoto hao wasome.

Dkt Nawanda ametoa Rai hiyo katika ziara yake Wilayani Maswa katika shule mpya ya Sekondari Dakama katika ukaguzi wa Miradi Wilayani humo.

"Kuna mchezo upo hapa katika Kata hii kuna baadhi ya Vijana wawili watatu wanaangalia angalia watoto wangu wale,Acheni nitawafunga miaka 30.Waache wasome tunataka akina Mama Samia wengine"

Aidha Dkt. Nawanda amemuagiza Mkuu wa POLISI Wilayani Maswa kufanya ufuatiliaji kuwabaini wale wote wanaojihusisha kimapenzi na Wanafunzi na kuwachukulia hatua ili kukomesha tabia hiyo.

"Na hili nimetoa tangazo OCD si upo hapa hakikisha wale wote ambao watabainika wanatembea na Wanafunzi lazima tuwachukulie hatua.Tunachotaka watoto wote wanaoanza Shule ya Msingi wanahitimu kwa Asilimia mia Moja isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu atawachukua Barabarani kwa sababu hao ni mapenzi ya Mungu"


www.simiyu.go.tz 

GCO,
Simiyu RS
27 Oktoba 2023

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post