TGNP YAMPONGEZA DR. TULIA KWA USHINDI MKUBWA KUWA RAIS WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI 'IPU'

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unampongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kwa ushindi mkubwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).


Kwa nafasi hii, Dr. Tulia amevunja rekodi kwa kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania, mwanamke wa kwanza Afrika na mwanamke wa tatu duniani kushika nafasi hiyo kwenye bunge lenye nchi wanachama 179 na wabunge 705 wanaoziwakilisha nchi zao.

Tunakuamini na kukutakia kila la kheri katika kufikia adhama yako ya kusimamia umoja kwa kuongeza ufanisi, uwajibikaji, uwazi na kulinda na kuhamasisha amani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments