WATENDAJI MADINI KUKUTANA KILA MWEZI KUJADILI MAENDELEO SEKTA YA MADINI

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde ameongoza kikao cha Watendaji wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini yake ikiwa ni utaratibu ulioanzishwa wa kukutana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kujadiliana utekelezaji wa majukumu, miradi pamoja na kufahamishana hatua mbalimbali zilizofikiwa katika Sekta ya Madini na masuala yanayohusu changamoto na maendeleo ya Sekta kwa ujumla.


Kikao hicho cha leo Oktoba 7, 2023, pia kimejadili na kutafakari ikiwemo kuweka mikakati itakayoongeza ushiriki wa Watanzania hususan vijana na wanawake katika Sekta ya Madini pamoja na kuongeza tija na thamani ya Sekta kwenye uchumi wa nchi na hatimaye mchango Pato la Taifa.


Aidha, Mhe. Mavunde amerejea kuhusu uwepo wa mpango mpya unaoitwa Madini kwa kesho bora (Mining for Brighter Tomorrow -MBT) ukiwa na lengo la kuwasaidia vijana, wanawake pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu kunufaika kupitia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amesema vikao hivyo vitasaidia kuifungua fursa kwa Watendaji wa Wizara na Wakuu wa Taasisi kutoa mawazo yao kwa kuwa vinajadili masuala muhimu na makubwa kuhusu Sekta ya Madini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post