MASELE AMPONGEZA DR .TULIA KWA USHINDI MNONO KUWA RAIS WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI


Dr. Tulia Ackson
Stephen Julius Masele
***
Makamu wa Rais mstaafu wa Bunge la Afrika (PAP) ambaye pia ni mbunge mstaafu wa jimbo la Shinyanga Mjini ndugu Stephen Julius Masele amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson ambaye amechaguliwa kwa kishindo kushika wadhifa wa Rais wa umoja wa Mabunge Duniani (Inter-parliamentary Union - IPU) ambayo makao makuu yake yako nchini Geneve Switzerland. 

Katika taarifa yake Mhe. Masele amemtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya. 

"Hakika ni heshima kubwa kwa nchi kupata nafasi kubwa katika siasa za kimataifa nampongeza sana Dr Tulia, hatua hiyo ni ushindi kwa taifa pia. Ni matumaini yangu Dr Tulia ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika siasa za kimataifa", amesema Masele. 


Masele ambaye pia amewahi kuwa mjumbe katika Bunge la Dunia amesema chombo hicho ni muhimu sana katika kuendeleza agenda zenye maslahi ya nchi na watu ulimwenguni kwa kuwa na kamati zenye nguvu sana kama kamati ya Haki za binadamu ambayo inasaidia sana kusimamia haki za binadamu ambazo zimekuwa na changamoto nyingi kwa siku za hivi karibuni. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments