BENKI YA CRDB SHINYANGA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA...YAAHIDI KUBORESHA ZAIDI HUDUMA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

BENKI ya CRDB Tawi la Shinyanga imeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, huku akiahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi.

Maadhimisho yao yamefanyika leo Oktoba 2,2023 katika benki hiyo ambayo yatakwenda hadi Oktoba 6 na yamehudhuriwa na wateja wake pamoja na kushiriki kifungua kinywa(Break Fast) na utoaji wa zawadi kwa baadhi ya wateja na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Meneja Tawi la Benki ya CRDB Shinyanga Luther Mneney, amewashukuru wateja kwa kuendelea kuiamini benki hiyo, huku akiahidi wataendelea na utoaji wa huduma bora zaidi.

"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja, na sisi Benki ya CRDB tumeanza kuadhimisha leo na wateja wetu, na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi," amesema Mneney.
Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana, amesema Benki hiyo inawathamini sana wateja wake, na mafanikio makubwa ambayo imekuwa ikiyapata ni kutokana na wao.

Aidha, amesema pale wateja wao wanapoona kuna changamoto mahali, wasisite kuwasiliana na benki hiyo ili kufanya marekebisho na kuendelea kutoa huduma bora kwao.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika wiki hiyo ya huduma kwa wateja Benki ya CRDB Jackton Koyi, ambaye ni mteja maarufu wa benki hiyo zaidi ya miaka 30, amewapongeza watumishi wa CRDB kwa kufanya kazi kwa weledi,bidii, ubunifu na kutoa huduma stahiki kwa wateja wake.

Ameiomba Benki hiyo ya CRDB waendelee na utoaji wa huduma nzuri na bora kwa wateja wao,sababu ni benki ambayo inafanya kazi vizuri ndani na nje ya nchi.
Mgeni Rasmi Jackton Koyi akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mjini Luther Mneney akizungumza kwenye Maadhimisho hayo ya wiki ya huduma kwa wateja Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza kwenye Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja Biashara CRDB Kanda ya Magharibi Anselm Mwenda akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mjini.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mjini Mwanahamisi Iddy akizungumza kwenye Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney akiwa na Mwenyekiti wa Mawakala wa huduma za kifedha mkoani Shinyanga Juliana Shilatu wakikata Keki kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mwenyekiti wa Mawakala wa huduma za kifedha Juliana Shilatu (kulia) akimlisha Keki Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney (kushoto)akimlisha Keki Mwenyekiti wa Mawakala wa huduma za kifedha mkoani Shinyanga Juliana Shilatu.
Muonekano wa Keki.
Wateja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Wateja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Wateja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meza kuu.
Watumishi wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.

Wateja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga wakishirikia kifungua kinywa (Break Fast).
Wateja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga wakipata kifungua kinywa (Break Fast).

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi Zawadi Mteja wa Benki hiyo Jackton Koyi.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa wateja wa Benki ya CRDB.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa watumishi wa Benki ya CRDB
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa Wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa wateja wa Benki ya CRDB.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post