WIZARA YA KILIMO, FAO, EU, SIDO NA AGRI THAMANI WAZINDUA VIBANDA VYA MSOSI ASILIA KATIKA SOKO LA KISUTU


Ijumaa tarehe 8 Septemba 2023, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Umoja wa Ulaya (European Union) wamekabidhi Vibanda 35 kwa Mama Lishe katika Soko la Kisutu, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili kupitia Kampeni ya Msosi Asilia inayotekelezwa na Agri Thamani kupitia Mradi wa Agri-Connect unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (European Union). Vibanda 35 vimetengenezwa na Shirika la SIDO.
Bw. Abebe Gabriel, Mkurugenzi Mkuu Msaidi na Mwakilishi wa Afrika wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) alisisitiza umuhimu wa Kampeni ya Msosi Asilia inayolenga kuhamasisha ulaji unaofaa kwa kutumia vyakula vya asili hapa nchini ili tuweze kuimarisha Lishe Bora nchini.

Aidha, pia Bw. Abebe Gabriel aliongezea kuwa ijapokuwa Tanzania ina chakula cha kutosha kwa asilimia mia moja (100%) lakini hii haimaanishi kwamba kila Kaya ina chakula hivyo inabidi tuweke utaratibu wa kuwa na bustani za mbogamboga katika Kaya zetu. Hii ni moja ya maeneo ambayo Agri Thamani imepata mafanikio makubwa Wilayani Bukoba, Kagera.

Kwa upande wake Mhe Mabhare Matinyi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke aliyekuwa anamwakilisha 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema “licha ya nchi kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100, lakini bado liko tatizo la utapiamlo kwa watoto ambalo ni matokeo ya lishe duni na madhara mengine ni pamoja na watoto kuathirika kiakili na baadae kuwa na kizazi ambacho kina mchango mdogo kwa taifa.

Shirika la Agri Thamani liliwashukuru sana Wizara ya Kilimo, FAO na EU kwa kuwapa fursa ya kutekeleza Mradi wa Msosi Asilia ambao mwaka huu Tamasha la Msosi Asilia linapangwa kufanyika Zanzibar na Mbeya, baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana Dar es Salaam.

Aidha, katika hafla hiyo, Mama Lishe walipika aina mbalimbali ta vyakula vya asili na wananchi walikula na kurahia na kuhamasika sana juu matumizi ya vyakula Asilia.

Kwa kuhitimisha, Mhe Mkuu wa Wilaya Mabhare Matinyi aliwaomba Mama Lishe waonyeshe muitikio mkubwa kwa kutumia Vibanda vya Kuuzia Msosi Asilia vilivyozinduliwa ili kuonyesha umuhimu wake kwa wahisani kwani Vibanda hivyo ni vya kisasa kabisa. Pia, Mhe Mkuu wa Wilaya aliwashukuru Wizara ya Kilimo, FAO , EU, SIDO na Agri Thamani Kwa kuwapa Thamani Mama Lishe.

#LisheBora #MsosiAsilia #LisheBoraNiMtaji

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post