WATANZANIA WATAKIWA KUWAOMBEA VIONGOZI


Na Mwandishi Wetu ,Dodoma

WANANCHI wameaswa kuwapongeza ma-Rais wote walioongoza Taifa la Tanzania  akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaiongoza serikali ya awamu ya sita kwa umahiri na weledi mkubwa katika kuhakikisha Taifa na wananchi kwa ujumla wanasonga mbele kimaendeleo.

Aidha wameaswa kumuheshimu na kumuombea Rais Samia  ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa weledi Zaidi ikiwa ni pamoja na kuwasimamia vyema viongozi waliopo chini yake.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa waelimishaji wazalendo kazi za Rais Samia ,Samwel chimanyi amesema,licha ya kazi kubwa anayoifanya Rais Samia lakini kuna watu ambao wamekuwa wakipotosha kwa makusudi na kusababisha viongozi walioongoza nchi hii kulaumiwa badala ya kupongezwa kwa uongozi wao madhubuti.

“Nikinukuu vitabu vya dini hasa Biblia kwa Imani ya dini yangu kitabu cha Warumi 13:1 kinasema ‘itiini Mamlaka inayowaongoza kwa kuwa hakuna Mamlaka isiyotoka kwa Mungu ,na hata hiyo iliyopo imetoka kwa Mungu,yeyote ashindanaye na Mamlaka hushindana na agizo la Mungu,

“Hayo ni maneno katika vitabu vya dini,kwa hiyo sisi kama watanzania ambao sifa yetu kubwa ni uzalendo na wapenda amani ,kama wapenda amani kazi kubwa tunapaswa wakati wote kujikumbusha habari ya kulinda na kumtunza amani yetu na Zaidi sana kuwaheshimu na kuwaombea.”amesema Chimanyi

Aidha amekemea wanaodai kuwa nchi inataka kuuzwa kutokana na uwekezaji wa Bandari unaotaka kuingiwa baina ya Tanzania na Dubai huku akisema Rais ana nia njema ya uwekezaji huo na siyo vinginevyo.

“Wanaomtukana Rais Samia na wasaidizi wake mimi ninaamini hawaelewi vizuri  baadhi ya mambo ,hata hao wanaotangaza maandamano chanzo chake ni kutoelewa nini  Rais anafanya kwa maslahi mapana ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo,

“Sasa sisi tumejitoa tunaenda kuelimisha wananchi wote kuhusu kazi anazozisimamia na anazozifanya Rais Samia ikiwemo kukamilisha miradi ya kimkakati ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR) ,Bwawa la Mwalimu Nyerere na miradi mingine mingi hapa nchini lakini pia kuendelea kusimamia amani na utulivu .”amesema na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo Mimi niseme kwamba tunajivunia nchi yetu Tanzania kwamba ni yenye amani na Dunia nzima wanafahamu hilo,kwa hiyo nawapongeza Viongozi wetu siyo Marais tu bali na viongozi wote waliokuwa chini yao wakiwemo mawaziri wakuu na Makamu wa Rais wastaafu ,makatibu wakuu na wengine wote,wamefanya kazi nzuri sana na ninaamini baada ya Elimu hiyo kutolewa kila mmoja ataona mambo mazuri yanayofanyika katika nchi hii.” Amesema na kuongeza kuwa

“Hapo nimeeleza kwa kifupi lakini tutakapoanza kuelimisha jamii,tutaeleza kwa kirefu kazi za Marais waliopita na kazi zinazoendelea kufanywa na Rais Dkt.Samia.”

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa watanzania wote kumuunga mkono Dkt.Samia katika mambo ambayo ya msingi sana ikiwa ni pamoja na anavyoendelea kulisimamia Taifa katika misingi ya amani na utulivu "

Akizungumzia  Ma-Rais watano waliotangulia ambao ni Ally Hassan Mwinyi,Hayati William Benjamin Mkapa,Jakaya Mrisho Kikwete na Hayati John Magufuli Chimanyi amesema, wote kwa pamoja wamefanya kazi kubwa na nzuri ikiwemo kulitoa Taifa mikononi mwa wakoloni,kujenga miundombinu ya barabara,kuimarisha miundombinu ya huduma za kijamii,ujenzi wa vyuo vikuu na ujenzi wa miradi ya kimkakati ambavyo vyote kwa pamoja Rais Samia aliyepo madarakani hivi sasa anaendeleza vizuri.amesisitiza Chimanyi na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo hao viongozi wetu pamoja na wale wote waliokuwa chini yao,bila kumsahau Rais wetu aliyepo madarakani ambaye anaongoza kwa kutumia akili Zaidi badala ya nguvu,tunapaswa kuwapongeza hasa Rais Samia ili kumpa ari Zaidi ya kuwatumikia watanzania.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post