SERIKALI YAENDELEA KUTILIA MKAZO SUALA LA ANWANI ZA MAKAZI




Na Dotto Kwilasa, Dodoma

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri  amesisitiza kuundwa kwa timu ya ufuatiliaji na tathmini ya zoezi la Anwani za Makazi  ili kufanikisha azma ya Serikali ya kila Mtu  kutambulika kirahisi mahali anapoishi.

Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa jamii kufikiwa na  huduma za Kijamii kwa haraka ikiwa ni pamoja na huduma za biashara mtandao kuboreshwa.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Dodoma  ameeleza hayo leo Sept  14,2023 Jijini Dodoma ,wakati akifungua mafunzo  ya siku mbili kuhusu Mfumo wa anwani za Makazi kwa Maafisa Tarafa,Maafisa Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa pamoja  na Maafisa Watendaji wa Mitaa wa Jiji la Dodoma.

Aidha mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano naTeknolojia ya Habari Kwa lengo la kuboresha huduma za jamii na kuhuisha maisha kidigitali.

Kwa Upande wake Mratibu wa anwani za Makazi Kitaifa,Panton Mbugi ameeleza kuwa  Mafunzo ni muhimu kwa kuwa yatalifanya Jiji la Dodoma kuwa la mfano katika kutekeleza zoezi hilo.


Nao washiriki wa mafunzo hayo,Wameishukuru Wizara ya Habari kwa mafunzo hayo na kuahidi kutekeleza kwa Vitendo.

Joshua Jembe ameeleza kuwa mafunzo ya anwani za makazi ni muhimu kwa Kila mtanzanzania Ili kurahisisha huduma za kijamii kwenda kidigitali na kutoka wakati.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post