MSANII JUX ANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA GARI

 
Mwimbaji Staa wa Bongofleva Juma Mussa Mkambala (JUX) pamoja na Wasaidizi wake wamenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea leo maeneo ya Nungwi Unguja Zanzibar wakielekea Kendwa Rocks baada ya Gari aina ya Coaster kufeli breki na kukosa mwelekeo kisha kulifuata gari walilokua wakisafiria msanii huyo na kuligonga ubavuni.

Meneja wa msanii huyo Raymond Maziku amesema ni Mtu mmoja tu aliyepata mshtuko kwenye ajali hiyo na kuwaishwa Hospitali lakini wengine wote wametoka salama kwenye ajali hiyo.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post