KIJANA MBARONI KWA MAUAJI YA BABA YAKE


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Antony Mkwawa

Na Joachim Nyambo, Mbeya.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia kijana aitwaye Humphrey Kihali[25] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya baba yake mzazi aitwaye Francis Kihali[50] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Antony Mkwawa awali Septemba 10, 2023 majira ya saa 10:45 jioni huko eneo la Ilemi mtuhumiwa alimvizia baba yake mzazi Francis Kihali akiwa chumbani kwake na kisha kumpiga kwa kutumia ubao ambapo alikimbizwa
Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na kufariki dunia leo Septemba 11, 2023 majira ya saa 1:30 asubuhi.

Kaimu Kamanda Mkwawa amesema pamoja na uchunguzi wa awali kubainisha kuwa mtuhumiwa ana tatizo la akili, uchunguzi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuate.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetoa wito kwa wazazi na walezi ambao wana changamoto ya watoto wenye matatizo ya Afya ya Akili kuchukua tahadhari kwa kuweka uangalizi madhubuti na kufuata maelekezo ya utumiaji wa dawa wanazopewa ili kuzuia madhara makubwa kama haya yasitokee.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post