MANISPAA TABORA YASAINI MKATABA UJENZI WA BARABARA KILOMETA 10


Na Mwandishi Wetu

MANISPAA ya Tabora imesaini mkataba wa ujenzi wa Barabara za kilometa 10 chini ya Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC).

Mkataba huo umesainiwa leo hii jijini Dar es Salaam mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa na kwa upande Manispaa mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Elias Kayandabila.

Wengine walioshuhudiwa utiwaji saini wa mkataba huo ni Meya ya Manispaa Ramadhani Kapela, Mbunge wa Jimbo la Tabora pamoja na Mwanasheria wa Manispaa Mwalukasa Robert Matungwa.

Mkandarasi wa Ujenzi ni M/s Chongqing International Construction Corporation kwa Gharama ya Sh.16,689,060,185.87 na Mkandarasi Mshauri M/s UNITEC Civil Consultants Ltd wakishirikiana na UWP Consulting (Tanzania) Ltd kwa gharama ya Sh. 1,472,345,999.44

Kutokana na kusainiwa kwa mkataba huo Manispaa ya Tabora imemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia TAMISEMI chini ya Waziri Mchengerwa kwa kuendelea kuboresha maisha ya wana Tabora Manispaa kwa kuwaboreshea niundombinu ya barabara na hivyo, kuboresha maisha yao.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post