BODI YA USHAURI TBA YATEMBELEA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA TBA MJI WA SERIKALI MTUMBA
BODI ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Arch. Dkt. Ombeni Swai kukagua na kujionea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA

BODI ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imepongeza kazi kubwa inayofanywa na TBA kutekeleza ujenzi wa ofisi mbalimbali za Serikali katika Mji wa Serikali.

Mwenyekiti wa Bodi Arch. Dkt. Ombeni Swai ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Bodi hiyo kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Pia, ametoa wito kwa TBA kuendelea kutumia wataalamu wa ndani kwa kuwaamini na kuwajengea uwezo ili TBA iweze kujenga Majengo mengi na makubwa.

"Kuliko hata haya na ikiwezekana tufanye nje ya Tanzania ikiwezekana tuitwe Rwanda ama Botswana kwenda kujenga na kusimamia Majengo kama haya,"amesema Dkt.Swai

Aidha Dkt.Swai amesema lengo la ziara hiyo ni kuona malengo yaliyowekwa na TBA jinsi yanavyotekelezwa kwa ufanisi

Amesema wametembelea majengo kadhaa ikiwemo Wizara ya kilimo na bahati nzuri mkandarasi amenunua vifaa vyote ambavyo vinahitajika na ubora wa kazi ni mzuri.

Wamepita katika jengo la Wizara ya Afya ambapo amedai ujenzi umefikia asilimia 94 na mkandarasi amenunua vifaa vya kumaliza jengo na amelipwa sehemu kubwa ya malipo yanayostahili.

"Quality (ubora) ya kazi tuliyokagua katika sehemu tofauti tofauti ni nzuri sana,tumemalizia katika Ofisi ya Rais Utumishi ni jengo linaongoza na limefikia asilimia 93.Kazi zilizobaki ni za kumaliza ambazo ni ndogo,"amesema Dkt.Swai

"Kwa ujumla miradi inaenda vizuri tunaimani kwa jinsi ambavyo Serikali inaendelea kutoa fedha itakamilika kwa wakati.

"Tunaipongeza sana Serikali ya Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambayo imetoa fedha kuhakikisha miradi hiyo inakwenda vizuri,"amesema Dkt.Swai

Amesema wanaendelea kumuomba Rais kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia yale Majengo ambayo bado yapo nyuma.

Aidha, ameishukuru TBA na Taasisi zingine kwa jinsi ambavyo zimefanya kazi nzuri.

Amesema miradi hiyo imeajiri watu wengi ambao ni wataalamu wa ndani ambao wengi ni vijana wa Kitanzania

"Hii inatupa faraja kubwa kwamba kazi ya Serikali kusomesha wataalamu wa ndani inaweza ikasaidia na huko mbeleni tukaondokana na utegemezi wa kutoka nje,"amesema Dkt.Swai

Naye Mkadiriaji Majenzi kutoka Idara ya Ushauri TBA Bi.Neema Kifua, amesema katika mradi huo wa Mji wa Serikali TBA, inasimamia ujenzi wa majengo 17, ambapo majengo 13 ni ofisi za wizara na majengo 4 ni ya ofisi za Taasisi za Serikali.

Awali Meneja wa Ujenzi TBA, Manase Shekalaghe ameeleza kuwa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Utumishi upo hatua za mwisho kukamilika.


BODI ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Arch. Dkt. Ombeni Swai kukagua na kujionea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


BODI ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Arch. Dkt. Ombeni Swai wakiendelea kupata maelezo kutoka kwa Mkadiriaji Majenzi kutoka Idara ya Ushauri TBA Bi.Neema Kifua, wakati wa ziara ya Bodi hiyo ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Kilimo lililotembelewa na Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Dkt. Ombeni Swai,akitoa maelekezo wakati wa ziara ya Bodi hiyo walipotembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Dkt. Ombeni Swai,akisikiliza taarifa ya miradi kutoka kwa Mkadiriaji Majenzi kutoka Idara ya Ushauri TBA Bi.Neema Kifua,wakati wa ziara ya Bodi ya Ushauri ya TBA walipotembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Dkt. Ombeni Swai,akitoa maelekezo wakati wa ziara ya Bodi hiyo walipotembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Afya lililotembelewa na Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma na Utawala Bora, lililotembelewa na Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Dkt. Ombeni Swai,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bodi ya Ushauri ya TBA kutembelea na kukagua Maendeleo ya baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Mkadiriaji Majenzi kutoka Idara ya Ushauri TBA Bi.Neema Kifua,akizungumza mara baada ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kufanya ziara ya kukagua na kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Meneja wa Ujenzi TBA, Manase Shekalaghe,akizungumza mara baada ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kufanya ziara ya kukagua na kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na TBA katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post