UWT YATOA SIKU 90 KUKAMILISHA MRADI WA MAJI


MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) na MNEC, Zainabu Shomari ameitaka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (MAUWASA) wilayani Maswa Mkoani Simiyu kuhakikisha wanakamilisha mradi wa maji ndani ya siku 90.


Akizungumza leo katika Ukaguzi wa mradi huu wa Maji ameitaka Mamlaka hiyo kutoa taarifa mbele ya Viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi kama mradi huo umeshindwa kutekelezeka kutokana na ukosefu wa fedha.


Amesema hajaridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umelenga kuwahudumia wananchi baada ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kuahidi kuwatua akina mama ndoo kichwani.


"Kama kuna tatizo lolote ambalo mnahisi linaleta mkwamo, hiki ni Chama Cha Mapinduzi na serikali yetu na viongozi ni wasikivu…hatupendelei kuona na kusikia kuna mkwamo wa mradi wa maji kwa kukosa fedha’’, alisema na kuongeza.


‘’Rais Samia amehakikisha analeta fedha kwa ajili ya kumtua mama ndoo kichwani, mnaona maeneo yote ya Tanzania yanafaidika…mkisema changamoto ni fedha, ninakuwa sielewi hasa katika suala la maji’’.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post